Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Jamuhuri John, mwenye umri wa miaka (28) amekutwa amejinyonga katika mti wa mbuyu baada ya kuwajeruhi kwa Panga mke na mtoto wake kisha kukimbia kusikojulikana.
Akizungumzia
tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Edmundi
Urio alisema tukio hilo la kujinyonga liligundulika mnamo tarehe
17/08/2012 majira ya saa 06:45 asubuhi, na wananchi waliokuwa
wakimfuatilia katika Kijiji cha Kikombo Kata na tarafa ya Kikombo Wilaya
ya Dodoma Mjini.
“Uchunguzi
wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha kujinyonga kwa mtu huyo ni ugomvi
wa mapenzi kwani marehemu alikuwa amewajeruhi mke na mtoto wake kwa
kuwakata na mapanga kisha kukimbia kusikojulikana hadi alipogundulika
amejinyonga.“ Alielezea Kamanda Edmundi Urio.
Bw.
Urio alieleza kwamba Marehemu alikuwa na ugomvi na mke wake kwa muda
mrefu kitu kilichopelekea mwanamke huyo kutoroka nyumbani kwake na
kukimbilia kwenda kuishi Tanga inakodaiwa kuwa ni kwa baba yake mzazi.
Kamanda
Edmund Urio alisema, baaada ya kukaa muda mrefu bila kumuona mke wake
marehemu alikuwa na wasiwasi kuwa ameolewa, hivyo aliamua kumtafuta mke
wake huyo na ndipo alipoamua kwenda kwa mtendaji wa Kijiji hicho cha
Kikombo Bw. Wenos Dede kuomba barua ya kumtafuta mke wake Tanga na
kupatiwa barua hiyo.
Aidh
Bw. Urio alieleza kwamba Jana majira ya saa mbili usiku marehemu na mke
wake wakiwa wanarudi toka Tanga walipewa maelekezo kwamba, wafike
kwanza kwa mtendaji kumjulisha na kwa usuluhishi zaidi,
walipofika hawakumkuta mtendaji kwa kuwa alikuwa amekwenda
kuhudhuria semina ya mambo ya Sensa katika Kijiji cha Ihumwa.
“Hivyo
wakiwa njiani walishindwa kuelewana, kwani mwanamke alikuwa anataka
kwenda kulala kwa bibi yake hapo hapo kijijini, ili kesho yake wamtafute
mtendaji ili wamalizane lakini mume wake alikataa na kumwambia amsubiri
akachukue shuka ndipo akakimbia nyumbani kwao akachukua Hengo na
kulificha katika koti kisha kurudi na kuanza kumshambulia mke wake.”
alieleza Kamanda Urio.
Kaimu
Kamanda huyo wa Mkoa wa Dodoma, alimtaja mwanamke huyo aliyejeruhiwa
kuwa nia Aksa John, mwenye umri wa miaka (21), mgogo na mkazi wa
Kikombo, pamoja na mtoto wake aitwaye Gerald John mwenye umri wa miaka
(4) aliyejeruhiwa kwa kukatwa Panga katika mguu wake wa kushoto.
Alisema
mwanamke huyo amejeruhiwa kwa kukatwa na panga mkono wa kulia chini ya
kiganja, na mkono wa kushoto kidole chake gumba kilikatwa kabisa pamoja
na kujeruhiwa katika mguu wa kushoto karibu na sehemu ya kukanyagia.
Kamanda
Urio Amesema majeruhi wote wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa
Dodoma, ambapo Mama huyo amelazwa katika wodi namba nane wakati mtoto
wake amelazwa wodi namba moja na kwamba wanaendelea vizuri.
No comments:
Post a Comment