Aaron Ramsey akifunga bao jana dhidi ya Korea ya kusini. |
Jamani huu ni mkosi au ni bahati mbaya tu inatokea?
Kila mchezaji wa Arsenal Aaron Ramsey anapofunga bao basi masaa kadhaa baadae kuna kifo cha mtu maarufu kinatokea. Hii ilianza wakati alipofunga bao dhidi ya Sunderland na masaa 24 baadae mwanamuziki Whitney Houstona akafariki dunia, na pale alipofunga goli la ushindi ya Manchester United - majeshi ya Marekani yakamuua Osama Bin Laden, Ramsey alipowatungua Tottenhm, mbunifu, mmiliki na aliyekuwa CEO wa kampuni inayotengeneza bidhaa za Apple ya Marekani akafariki dunia, na tena alipowafunga Marseille kwenye Champions league - Colonel Maamar Gaddafi akauwawa na majeshi ya waasi nchini kwake Libya.
Marehemu - Kirk Urso |
source http://www.shaffihdauda.com/
No comments:
Post a Comment