Pages

Monday, August 6, 2012

BAADA YA AARON RAMSEY KUFUNGA BAO JANA - MTU MWINGINE MAARUFU AFARIKI DUNIA


Aaron Ramsey akifunga bao jana dhidi ya Korea ya kusini.

Jamani huu ni mkosi au ni bahati mbaya tu inatokea?
Kila mchezaji wa Arsenal Aaron Ramsey anapofunga bao basi masaa kadhaa  baadae kuna kifo cha mtu maarufu kinatokea. Hii ilianza wakati alipofunga bao dhidi ya Sunderland na masaa 24 baadae mwanamuziki Whitney Houstona akafariki dunia, na pale alipofunga goli la ushindi ya Manchester United - majeshi ya Marekani yakamuua Osama Bin Laden, Ramsey alipowatungua Tottenhm, mbunifu, mmiliki na aliyekuwa CEO wa kampuni inayotengeneza bidhaa za Apple ya Marekani akafariki dunia, na tena alipowafunga Marseille kwenye Champions league - Colonel Maamar Gaddafi akauwawa na majeshi ya waasi nchini kwake Libya.

Marehemu  - Kirk Urso
Ikiwa imepita miezi kadhaa wakiwa hajafunga bao, jana akiwa anaiwakilisha timu ya taifa ya Uingereza kwenye michuano ya Olympic katika hatua ya robo fainali Ramsey akafunga bao, na kama ilivyo ada asubuhi ya leo klabu ya Columbus Crew ya Marekani imetangaza kwamba mchezaji wake Kirk Urso amefariki akiwa na miaka 22.
                                           source http://www.shaffihdauda.com/

No comments:

Post a Comment