Hatimaye mchezaji wa Bolton Fabrice Muamba ametangaza kuachana na soka leo hii kutokana na ushauri wa daktari.
Mchezaji huyo mwenye asili ya Congo, alipata mshtuko wa moyo wakati wa mechi ya FA Cup dhidi ya Tottenham, amesema ana uchungu mkubwa kuachana na kucheza soka lakini hana budi zaidi ya kuweka mbele afya yake.
Muamba ameishukuru sana timu ya madaktari kwa kuokoa maisha yake na ameshukuru kwa maombi na sapoti kubwa aliyoipata kutoka kwa wapenzi wote wa soka duniani.
Moyo wa Muamba ulisimama kwa saa 78 baada ya kudondoka kwenye dimba la White Hart Lane baada ya kupatwa mshtuko wa moyo hali iliyopelekea kufanyiwa matibabu na kuweza kuokoa maisha yake.
Alikaa mwezi mzima Hosptali lakini aliwashangaza madaktari kwa jinsi alivyopata nafuu kwa haraka huku akisistiza anataka urudi kwenye dimba aendelee kucheza soka.
Kiungo huyo wa Bolton na England alienda mpaka nchini Ubelgiji wiki iliyopita kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji mdogo ili kuweza kuwa fiti kwa ajili kurudi uwanjani.
Mchumba wake Shauna ali-tweet kuwaambia mashabiki wa Muamba kwamba operation imeenda vizuri na atarudi kucheza soka kwa nguvu kuliko ilivyokuwa mwanzoni, lakini siku moja baadae madaktari wakampa taarifa mbaya kwamba kurudi kucheza soka kutahatarisha maisha yake kwa kuwa moyo wake hauwezi kuhimili.
Kabla ya kutangaza kustaafu Mumba aliwaambia mashabiki wake waendelee kutabasamu na kila kitu kitakuwa poa.
Historia yake ya soka na kuanza kujulikana ilianzia katika academy ya soka ya Arsenal mwaka 2002 kabla ya kuhamia Birmingham na baadae akaenda Bolton mwaka 2008.
No comments:
Post a Comment