Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk Willbroad Slaaa, amefukuzwa katika nyumba ya kulala wageni ndani chuo cha Ufundi stadi (VETA) Mikumi wilayani kilosa mkoani Morogoro kwa kile kilichoelezwa kuwa ni sababu za kisiasa ikiambatana na kuzimwa kwa umeme kwa mji mzima.
Dkt. Slaa ambaye aliwasili majira ya saa 8.00 mchana katika mji wa mikumi akitokea tarafa ya malinyi wilaya Ulanga katika Operesheni yake ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) ikiwa ni muendelezo wa Operesheni Sangara.
Baada ya kuwasili hotelini hapo Dkt. Slaa alikabidhiwa funguo ya sehemu ya kufikia kutoka kwa Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa CHADEMA, Alfred Lwakatare na kuingia chumbani.
Ghafla alitokea meneja wa hoteli hiyo na kumueleza Dkt. kuwa sehemu hiyo imeshawekewa oda na wateja wengine na hivyo kutakiwa kutakiwa kuondoka katika eneo hilo mara moja.
Hata hivyo Dkt. Slaa alihoji ni kwanini mmoja wa husika wake ambaye ni Mwalimu wa anayefundisha VETA ambaye aliacha majukumu yake na kwenda kuhusika katika majukumu ya hoteli kumuhudumia eneo lenye vyumba vitatu likiwa na thamani ya sh. 75,000 kwa kila chumba kimoja sh. 25,000.
Hata hivyo meneja huyo aliendelea na kung’ang’ania Dk Slaa ni lazima aondeke kwakuwa yeye hakuwa na taarifa na ujio wake na hivyo kumlazimu kuondoka katika eneo hilo.
Akizungumzia hali hiyo, Dkt. Slaa alisema kuwa kuna mipango imefanywa na Serikali ya chama tawala ikiwa ni njia mojawapo ya kumdhoofisha katika kampeni za kuwakomboa Watanzania, “Kama mimi nafanyiwa mambo hayo kwa suala dogo la maladhi tu na Serikali ya CCM, je nyinyi wengine mtafanyiwaje?, Mnapaswa kujifirikia mara mbili,” alisema Dkt. Slaa.
Baada ya tukio hilo kutokea na Dkt. Slaa kuamua kuelekea katika eneo la mkutano gafla umeme ulizimwa katika mji wa mikumi hali ambayo ilitafsiriwa ni muendelezo wa hujuma dhidi ya CHADEMA huku wananchi wakidai mji huo haukuwa kuwa na tatizo hilo la umeme.
Kwa upande wake meneja wa Shirika la Umeme (TANESCO) mkoa wa Morogoro, Deogratius Ndamugaba, akijibu shutma za kukatika kwa umeme katika mji huo alisema kuwa kukatika huko kwa umeme kulitokana na hitilafu za kawaida na siyo hujuma au msukuma wa kisiasa, “Kukatika kwa umeme mikumi si kwa sababu ya CHADEMA ila ni feeder ya mikumi iko nje tangu saa 12.45 jioni, nguzo imeanguka na inapashwa kubadilishwa na sehemu yenyewe ni porini, kuna giza na chui,” alisema Meneja huyo.
Alisema kuwa amekuwa akijaribu kuwasiliana na vyombo vya habari ili kuwapa taarifa wananchi wa Mikumi na kwa utendaji kazi wa eneo hilo kwa muda huo ulionekana kuwa mgumu na kwamba tayari mafundi wa Tanesco walikuwa katika eneo la tukio kufanya malekebisho.
SOURCE SANGA FESTO
No comments:
Post a Comment