Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, August 7, 2012

JAMBAZI ALIYETOKA KWA MSAHAMA WA RAIS KIKWETE ANUSURIKA KUUWAWA KWA WIZI WA PIKI PIKI TAZAMA JINSI ALIVYOPIGWA NA WANAINCHI



Kijana mtuhumiwa wa wizi wa piki piki Mohamed akivuja damu kwa kichapo na akiandaliwa kuchomwa moto kabla ya kuokolewa na polisi
Polisi wakimwokoa mtuhumiwa wa wizi wa piki piki
Mke wa mtuhumiwa akichezea kichapo kwa wizi
Mtuhumiwa wa pili wa wizi wa piki piki
mtuhumiwa wa wizi wa piki piki Mohamed Chambogo akichezea kichapo
Hapa akiwa hoi na kuwekwa katika buti ya gari ndogo kwa ajili ya kwenda mafichoni kuteketezwa kwa moto kabla ya kuokolewa na polisi
Kipigo kikiendelea kutoka kwa wananchi wenye hasira kali wakazi wa Ikonongo Mkwawa
Kijana anayedaiwa ni mmiliki wa piki piki iliyoibwa (kushoto)

WATUHUMIWA wawili akiwemo mmoja ambaye ni jambazi alitolewa kwa msahama wa Rais Jakaya Kikwete mwaka jana Mohamed Chambogo mkazi wa Ikonongo katika Manispaa ya Iringa amenusurika kuuwawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kutuhumiwa kuiba pikipiki mpya na kusambaratisha na kuiuza kuipima katika mzani na kuiuza kama vyuma chakavu kwa kiasi cha shilingi 20,000 pekee.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa sharti la kutotaja majina yao vijana hao ambao walikuwa wakimwadhibu mtuhumiwa huyo walisema kuwa wamelazimika kutaka kumuua kwa kumchoma moto kijana huyo baada ya kuchoshwa na tabia zake za wizi na kuwa hii ni mara ya tatu ananusurika kuuwawa na kuwa awamu ya kwanza alikatwa sehemu zake za siri kwa tuhuma kama hizo.

Wananchi hao walisema kuwa piki piki anayotuhumiwa kuiba ni ya mkazi mwenzao wa eneo hilo na iliibiwa toka mwezi wa tatu mwaka huu na baada ya kutafutwa bila mafanikio jana ndipo walipobahatika kuona mabaki ya piki piki hiyo katika chumba cha mtuhumiwa huyo.

Kwani walisema kuwa mabaki ya piki piki hiyo yalionekana baada ya mkazi mmoja wa eneo hilo la Ikonongo kata ya Mkwawa kuibiwa mahindi yake kama debe moja hivi na katika msako wa kusaka mahindi hayo ndipo waliposhuhudia mabaki ya piki piki hiyo ambayo chesesi namba yake ilionyesha ni ile ambayo ilikuwa imeibwa kwa mkazi wa eneo hilo.

Hivyo walisema baada ya hapo msako mkali ulianza kwa wanakijiji wote na kufanikiwa kumkamata kijana huyo muda wa saa 1 usiku wakati akirejea kutoka mafichoni akiwa na mali nyingine zinazodhaniwa kwa ni za wizi na ndipo wananchi walipoanza kumpa kichapo na kutaka kumchoma moto kabla ya jeshi la polisi kufika kumuokoa.

Diwani wa kata hiyo ya Mkwawa Thobias Kikula akielezea tukio hilo alisema kuwa katika kata hiyo kumekuwepo na matukio mbali mbali ya uharifu na kuwa tayari mkakati wa pamoja wa kupambana na waharifu hao umewekwa.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamuanda alithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na kuwa jeshi lake bado linachunguza zaidi mtandao huo wa uharifu mkoani hapa na kuwapongeza wananchi hao kwa kukamata salama bila kuua watuhumiwa hao wawili.
MWISHO

No comments:

Post a Comment