Yanga mazoezini
MABINGWA wa soka Afrika Mashariki na Kati, Yanga ya Dar es Salaam wanatarajiwa kuanza tena mazoezi leo saa 3:00 asubuhi kujiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu.Kocha Mkuu wa klabu hiyo, Mbelgiji Tom Saintefiet Aamesema j kwamba baada ya mapumziko ya siku tano tangu watwae Kombe la Kagame, leo wanaanza tena kujiandaa na Ligi Kuu.Tom amesistiza wachezaji wote wanatakiwa kuripoti mazoezini Uwanja wa Kaunda, uliopo makao makuu ya klabu hiyo, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani.Yanga ilitwaa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Jumamosi kwa kuifunga Azam FC mabao 2-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wafungaji Hamisi Kiiza ‘Diego Milito’ na Said Bahanuzi ‘Spider Man’.Hilo lilikuwa taji la tano la michuano hiyo kwa Yanga kihistoria, baada ya awali kutwaa mataji ya Kombe hilo katika miaka ya 1975 Zanzibar, 1993, 1999 Uganda na 2011 Dar es Salaam na mara zote hizo, ikiwa chini ya makocha wa kigeni.Mwaka 1975 Yanga ilibeba Kombe hilo, ikiwa chini ya kocha kutoka Jamhuri ya Kodemokrasia ya Kongo (DRC), Tambwe Leya (sasa marehemu), 1993 chini ya kocha kutoka Burundi, Nzoyisaba Tauzany pia marehemu, 1999 chini ya Raoul Shungu kutoka DRC na mwaka jana chini ya Mganda Sam Timbe.Mapema juzi ziliibuka habari kwamba, baada ya kuipa Yanga Kombe la Kagame,Tom ameomba kazi ya kufundisha timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, lakini mwenyewe alisema baadaye akizungumza na BIN ZUBEIRY kwamba tangu amejiunga na klabu hiyo mwezi uliopita hajawahi kuomba kazi sehemu nyingine yoyote.Mtakatifu Tom alisema anashangazwa mno na habari hizo za kizushi, za kizandiki zenye kulenga kumchonganisha yeye na mwajiri wake, Yanga SC.“Nakumbuka niliwahi kuomba kazi Chama cha Soka Kenya (KFF) kufundisha timu yao ya taifa (Harambee Strars), lakini ilikuwa ni muda mrefu sana hata kabla sijaomba kazi Yanga,”alisema.Blog moja iliyowahi kuandika Iddi Kipingu anagombea Uenyekiti Yanga, jana iliandika habari yenye kichwa kisemacho; “WIKI MOJA BAADA YA KUIPA UBINGWA: KOCHA WA YANGA TOM SAINTFIET ATUMA MAOMBI YA KUIFUNDISHA HARAMBEE STARS,”.Akiizungumzia habari hiyo, Mtakatifu alisema; “Ni uongo, tangu nimesaini mkataba na Yanga, sijawahi kuomba kazi pengine popote,”alisema.
VYUO VYAASWA KUWA NA WALIMU WANAOFUNDISHA WATU WENYE MAHITAJI MAALUMU
-
CHUO cha Furahika Education College kilicho chini ya Mamlaka ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kimewaasa wakuu wa vyuo vyote nchini kuwa na
Wali...
25 minutes ago
No comments:
Post a Comment