Malawi
imekataa kuitikia wito wa Tanzania kutaka isimamishe shughuli za
kutafuta mafuta na gesi ziwa Malawi, wakati suluhu ya mvutano wa mpaka
ikisubiriwa.
Mvutano
wa maneno umezuka kati ya nchi hizo mbili baada ya Malawi kuipa leseni
Kampuni ya Uingereza kufanya utafiti katika eneo hilo.
Taarifa zinazohusiana
Maafisa
nchini Tanzania wanasema mvutano huo uliodumu kwa miaka 50 sasa unaweza
kuwa mkubwa iwapo ugunduzi wa mafuta na gesi utatokea kwenye ziwa hilo
linalojulikana kama Ziwa Nyasa nchini Tanzania.
Tanzania inasema inaendelea kufanya mazungumzo na Malawi na iko Tayari kulipeleka suala hilo kwenye vyombo vya upatanishi.
"Hili
ni suala nyeti sana na tungependa litatuliwe kwa maelewano, tutaendelea
na mazungumzo," Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania alisema.
Membe
wiki iliyopita alviambia vyombo vya habari nchini humo kuwa "shughuli
za uchimbaji katika eneo la kaskazini mashariki mwa ziwa hazina budi
kusitishwa kupisha mazungumzo kutatua mzozo huo yafanyike."
Malawi, koloni la zamani la Uingereza, kwa upande wake iliapa kuendelea na chughuli za utafiti wa hewa gesi mkaa (hydrocarbons).
Tanzania,lililotawaliwa
na Ujerumani na baadaye Uingereza, inadai kuwa sehemu ya kilometa za
mraba 29,600 sawa na maili 11,400 za ziwa, wakati Malawi inarejea
makubaliano ya mwaka 1890 yanaonyesha kuwa mpaka kati ya nchi hizo mbili
uko kwenye ufukwe upande wa Tanzania.
Msumbiji pia inadai ina sehemu yake katika ziwa hilo la tatu kwa ukubwa barani Afrika.
Mwezi
Septemba mwaka jana serikali ya marehemu Bingu wa iliipa leseni kampuni
ya Surestream Petroleum, kutafiti mafuta na gesi ziwani.
Mataifa hayo mawili yatafanya mazungumzo juu ya mpaka kaskazini mwa Malawi katika mji wa Mzuzu Agosti 20 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment