Mtibwa Sugar 2009 |
Na Prince Akbar
MTIBWA Sugar imeanza vema michuano ya Kombe la BancABC Super
8 baada ya kuifunga Polisi, zote za Morogoro mabao 2-0 kwenye Uwanja wa
Ushirika mjini Moshi, Kilimanjaro jioni ya leo.
Mabao ya Mtibwa, inayofundishwa na mchezaji wake wa zamani, Mecky
Mexime yalitiwa kimiani na Vincent Barnabas dakika ya 39 na Yussuf Bida dakika
ya 49, wakati la Polisi lilifungwa na Nicholas Kabipe mapema tu dakika ya 10.
Mechi hiyo ilipangwa kufanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri
Abeid mjini Arusha jana, lakini Menejimenti ya Uwanja huo ilizizuia timu zikiwa
getini na kudai hawana taarifa za mashindano hayo.
Jana ilielezwa mechi hiyo ingechezwa leo kwenye Uwanja wa General
Tyre mjini humo, badala ya Sheikh Amri Abeid, lakini imeshindikana na kuchezwa
Moshi.
Katika mechi zilizochezwa jana, mapema jioni Simba B ilitoka
sare ya 1-1 na Jamhuri ya Pemba kwenye Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam
katika mechi ya Kundi A. Jamhuri ndio waliotangulia kupata bao kupitia kwa
Bakari Khamis dakika ya 48, akiunganisha krosi ya Abdallah Othman, kabla ya
Shomary Kapombe, mchezaji pekee wa Simba A aliyecheza, kuisawazishia timu yake
kwa penalti dakika ya 83, baada ya Miraj Adam kuangushwa kwenye eneo la hatari
na Mfaume Shaaban.
Mechi iliyofuatia usiku Uwanja wa Amaan, Zanzibar, Azam FC
iliifunga Super Falcon mabao 2-0, wafungaji Abdi Kassim Sadallah ‘Babbi’ dakika
ya 20 na Joseph Lubisha Kimwaga, wa Azam B dakika ya 60.
Michuano hiyo ina makundi mawili, ikishirikisha timu nane,
Kundi A likiwa na timu za Simba, Jamhuri, Zimamoto na Mtende FC, wakati Kundi B
kuna Super Falcon, Azam FC, Mtibwa Sugar na
Polisi Moro na bingwa wa michuano hiyo inayodhaminiwa na Bank ABC
ataondoka na Sh. milioni 40, mshindi wa pili Sh. milioni 20, wa tatu Sh.
milioni 15 sawa na wa nne, wakati washiriki wengine wataondoka na Sh. Milioni 5
kila moja.
Michuano itachezwa katika vituo vinne vya Dar es Salaam,
Zanzibar, Arusha ambako imekataliwa na Mwanza, ambapo timu zitasafirishwa kwa
ndege kwenda kucheza mechi katika vituo vyote. Kila timu itacheza mechi mechi
katika vituo vituo vitatu tofauti. Simba baada ya mechi ya jana, itakwea pipa
kwenda Arusha kucheza dhidi ya Mtende FC Alhamisi na itasafiri kwenda Mwanza
kwa ajili ya mechi yao ya mwisho ya Kundi A dhidi ya Zimamoto Jumamosi.
SOURCE http://bongostaz.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment