Pages

Friday, August 31, 2012

MWANAMUZIKI CHRIS WA MAREKANI AFARIKI KWA KUJIPIGA RISASI.


CHRIS LIGHTY AKIWA NA DIDDY
Mwanzilishi na mmiliki wa Violator Entertainment anayefahamika kwa jina la Chris Lighty ambaye pia alikuwa mwanamuziki wa HipHop amefariki dunia siku ya Agosti 30 huko Marekani. Chriss alifariki baada ya kujipiga risasi ya kichwa kutokana na tafrani iliyokuwa ikimsumbua baina yake yeye na mkewe chanzo kikiwa ni upotevu wa fedha na madeni yanayoikabili familia hiyo, Chris ambaye alikuwa akidaiwa $5 milioni na IRS alilazimika kuuza baadhi
ya vitu vyake ikiwa pamoja na hotel ili kuweza kulipa deni hilo hali iliyomfanya kuonekana kama amechanganyikiwa na muda mwingi walikuwa hawaelewani na mkewe Veronica. Chris hatasahaulika kwa kuviinua vipaji ambavyo kwasasa ndio nguli wa muziki duniani kama vile; 50 Cent, Maria Carey, Busta Rhymes, Diddy, Jarule na wengineo

No comments:

Post a Comment