Pages

Friday, August 10, 2012

SIMBA YANG'ARA SUPER 8, AZAM YAPIGWA NA MTIBWA NYUMBANI




SHUJAA WA SIMBA; Christopher Edwar

SIMBA SC jioni imepata ushindi wa kwanza katika michuano ya BancABC Sup8r kwenye Uwanja wa Ushirika mjini Moshi, baada ya kuifunga Mtende FC ya Zanzibar mabao 2-0.
Simba, ambayo kwenye mechi ya kwanza ililazimishwa sare ya 1-1 na Jamhuri ya Zanzibar pia, mabao yake katika mchezo wa leo yalifungwa na Christopher Edward dakika ya 11 na 26 kwa penalti.
Mtende walilazimika kumaliza pungufu mechi hiyo, baada ya mchezaji wake, Rajab Mzee kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 86 kwa kumtolea lugha chafu refa wa kike, Judith Gamba.
Simba inatumia kikosi chake cha pili kwenye mashindano haya, ambacho kipo chini ya kocha Suleiman Abdallah Matola, Nahodha wa zamani wa Simba SC.
Katika mchezo mwingine uliofanyika kwenye Uwanja wa Chamazi, wenyeji Azam walifungwa mabao 2-0 na Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Mabao yote ya Mtibwa yalipatikana kipindi cha pili, wafungaji wakiwa ni Shaaban Kisiga ‘Malone’ na Hussein Javu.
Mtibwa iliyoifunga Polisi Moro 2-0 kwenye mchezo wa kwanza, sasa inaongoza kundi hilo kwa pointi zake sita, ikifuatiwa na Azam yenye pointi tatu, ambayo katika mchezo wake wa kwanza, iliifunga Super Falcon 2-0.
NA BIN ZUBEIRY 

No comments:

Post a Comment