Pages

Wednesday, August 15, 2012

STARS 3-3 BOTSWANA




TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imelazimisha sare ya kufungana mabao 3-3 na wenyeji Botswana mjini Gaborone katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa ulio kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Katika mchezo huo, mabao ya Stars yalifungwa na Mwinyi Kazimoto, Erasto Nyoni ambaye baadaye alitolewa nje kwa kadi nyekundu na Mrisho Ngassa.
Stars inatarajiwa kurejea Dar es Salaam kesho baada ya mechi hiyo, na wachezaji wa timu hiyo kujiunga na klabu zao, kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
na bin zubeiry

No comments:

Post a Comment