JESHI
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limetangaza kupiga mizinga 21
leo kuanzia saa 3.00 asubuhi katika maeneo ya Kigamboni jijini Dar es
Salaam, hivyo kuwataka wananchi kutokuwa na hofu kwani haitakuwa na
madhara yoyote kwao.
Taarifa
ya Kurugenzi ya Habari na Uhusiano ya jeshi hilo iliyotolewa jana,
imeeleza kuwa mizinga hiyo itapigwa mara baada ya kuwasili kwa meli za
kivita tatu kutoka nchini Japan.
Meli
hizo kutoka Jeshi la Wanamaji la Japan zinazoongozwa na Kamanda wa
Mafunzo wa Vikosi vya Wanamaji, Hidetoshi Funchinoue, atakayefuatana na
mabaharia 1,176 zitawasili leo asubuhi.
Imeelezwa
kuwa lengo la ugeni huo ni kufanya ziara ya kimafunzo kwa maofisa
wanafunzi waliomaliza masomo katika chuo cha Japan Maritine Self Defence
Forces (JMSDF).
“Mara
zitakapowasili meli hizo katika bandari ya Dar es Salaam itapigwa
mizinga 21 na pia kiongozi wa meli hizo atazungumza na waandishi wa
habari. Sherehe za mapokezi ya meli hizo zitaudhuriwa na Balozi wa Japan
nchini na makamanda wa JWTZ,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo, baada ya kuwasili ujumbe wa meli hizo
utatembelea bandari ya Dar es Salaam, kwa Meya wa Jiji na Makao Makuu ya
Navy, Kigamboni.
No comments:
Post a Comment