Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, September 29, 2012

HIACE YAWAKA MOTO MOROGORO, WASAMARIA WAUZIMA


 Gari hilo baada ya kushika moto.
 Dereva wa hiace hiyo akijaribu kuzima moto.
Baadhi ya abiria waliokuwa ndani ya Hiace wakishuhudia moto huo ukizimwa.
ABIRIA na dereva wa gari aina ya Toyota Hiace yenye namba za usajili T224 ADZ inayofanya safari zake kati ya mjini Morogoro na Bigwa, leo mchana wamenusurika kuungua kwa moto baada ya gari hilo kushika moto eneo la mlima wa Kwa Mnyonge jirani na kiwanda cha mifuko ya nailoni cha Ladwa. 
Moto huo ulizimwa na Wasamaria Wema kufuatia tukio hilo ambapo dereva aliwahi kuzivua nguo zake zilizokuwa zimeanza kushika moto ulioanzia kwenye injini. Dereva huyo hakupata madhara yoyote.

No comments:

Post a Comment