Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, September 26, 2012

KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA ATAKA VITA VIKOMESHWE NCHINI SYRIA.



Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon (pichani) ametoa wito kwa nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kuacha tofauti zao na kumuunga mkono mjumbe wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Lakhdar Brahimi, katika juhudi zake za kuusuluhisha mgogoro wa Syria.
Katika hotuba yake mbele ya baraza kuu la Umoja wa Mataifa, Bw. Ban Ki-Moon amezitahadharisha nchi wanachama kwamba hali nchini Syria imezorota kupita kiasi.
Amesema ukatili mkubwa na ukiukaji wa haki za binadamu unaendelea, ukifanywa hasa na upande wa serikali, lakini na upande wa waasi pia.
Shirika la kuchunguza haki za binadamu nchini Syria lenye makao nchini Uingereza, linakadiria kwamba watu wapatao 30,000 wamekwishauawa nchini humo tangu mgogoro huo ulipoanza takriban miezi 18 iliyopita.

No comments:

Post a Comment