Hamisi Kiiza 'Diego' |
Na Mahmoud Zubeiry
HAMISI Kiiza
‘Diego’ amerejea jioni hii mjini Dar es Salaam, akitokea kwao, Uganda ambako
alikuwa ana majukumu ya kitaifa na tayari amejiunga na wenzake kwa ajili ya
mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, dhidi ya Prisons mjini Mbeya
mwishoni mwa wiki.
Kiiza hakuwa
na Yanga kwa takriban wiki mbili, akiwa kwao kwa ajili ya kuichezea timu yake
ya taifa, The Cranes mechi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la
Mataifa ya Afrika mwakani nchini Afrika Kusini.
Katika mechi
hiyo iliyochezwa Jumamosi mjini Lusaka dhidi ya wenyeji, Zambia, Koronga wa
Uganda alifungwa 1-0 na sasa anahitaji ushindi wa 2-0 katika mchezo wa
marudiano nyumbani, ili kusonga mbele.
Kiiza ni
mmoja kati ya wapachika mabao hodari, ambao kocha Mkuu wa Yanga, Mbelgiji Tom
Saintfiet ‘Mtakatifu Tom’ anajivunia na amesema kwamba anatarajia mvua ya mabao
katika mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kutokana na uwezo mkubwa wa
kufunga wa wachezaji wake, kuanzia mabeki, viungo hadi washambuliaji.
Akizungumza
na BIN
ZUBEIRY jana, Mtakatifu Tom alisema kwamba mbali na washambuliaji
kufunga, pia mabeki wake na viungo wanafunga pia, na hilo linampa faraja sana.
Jana Yanga
ilicheza mechi ya mwisho ya kujipima nguvu kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu na
kushinda mabao 4-0 dhidi ya Moro united, Mrundi Didier Kavumbangu akifunga
mawili, mengine beki Juma Abdul na kiungo Shamte Ally.
“Kavumbangu aliwahi
kufunga pia tulipocheza na Sinza Stars, ninafurahia hilo, ni muhimu kwa klabu
kubwa, lakini pia wachezaji wengine wanaweza kufunga, Stefano Mwasyika, Nadir
Haroub ‘Cannavaro’, Juma Abdul…tumecheza mechi 14 kabla ya ligi, zikiwemo dhidi
ya Sinza Stars na Kijitonyama Stars, tumefunga mabao 42 na tumefungwa sita
tu,”alisema Mtakatifu Tom.
Saintfiet alitaka
mechi moja dhidi ya timu inayocheza kama wapinzani wao wa kwanza katika Ligi
Kuu, Prisons na pia katika Uwanja mbaya kama ambao atachezea mechi ya kwanza ya
ligi hiyo, Sokoine mjini Mbeya na ndiyo maana timu hiyo ikacheza na Moro United
juzi kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kijitonyama.
Saintfiet
ameridhika na kiwango cha timu na sasa anasema timu iko tayari kwa Ligi Kuu,
akianza na Prisons iliyorejea Ligi Kuu msimu huu kwenye Uwanja wa Sokoine, Septemba
15.
Hiyo ilikuwa mechi ya 11, Saintfiet anashinda
Yanga katika mechi 12 tangu ajiunge nayo miezi miwili iliyopita, mbali ya ziwe
za mazoezini dhidi ya Sinza Stars na Kijitonyama Stars.
Ndani ya mechi hizo kuna mechi sita za
Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, ambalo
aliiwezesha Yanga kutwaa ubingwa wa tano wa michuano hiyo, ikipoteza mechi moja
tu ya kwanza dhidi ya Atletico ya Burundi, kwa kufungwa 2-0, mabao yote ya
Kavumbangu, ambaye baadaye ikamsajili.
source http://bongostaz.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment