Pages

Thursday, September 6, 2012

MAJAMBAZI YAKAMATWA ARUSHA



Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Bw.Liberatus Sabas akiwa anawaonyesha waandishi wa habari risasi,pisto na kifaa cha kunyooshea risasi jana ofisini kwake.

 Wanachi wakiwa wanaangalia mwili wa marehemu mara baada ya kugongwa na gari jana katika barabara ya katimakutano jijini Arusha
Mahmoud Ahmad,Arusha
Jeshi la polisi mkoani Arusha limefanikiwa kuwakamata majambazi sugu watatu kwa nyakatitofauti wakiwa na silaha aina ya pisto yenye risasi tano pamoja na mashine ya kunyooshea bunduki , kifaa cha kubustia risasi pamoja na risasi 46 za bunduki aina ya smg Katika matukio mawili tofauti.

Akiongea na waandishi wa habari mkoani hapa kamanda wa polisi mkoa  wa Arusha Liberatus Sabas alisema kuwa matukio hayo mawili yalitokea  kwa nyakati  tofauti Katika maeneo tofauti ya mkoani hapa kufuatia msako mkali uliokuwa ukifanya na jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi wasamaria wema.

Kamanda alisema kuwa Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa ni jambazi sugu aliyejihusisha na matukoi ya hivi karibuni aliyefahamika kwa jina la Salimu Kiwele alimaarufu kwa jina la Msaula(39)mkazi wa sombetini mkoani hapa akiwa na mke wake  aliyetambulika kwa jina la Princes Juma (34) wote ni wakazi wa sombetini wamekamatwa   nyumbani kwao wakiwa na silaha pamoja na risasi.

Alisema kuwa watu hao walikamatwa wakiwa na silaha aina ya pisto  Glock FFN 350 ikiwa na risasi tano ambazo zilikuwa ndani ya magazine ya silaha hiyo.

Alisema kuwa mtu  huyu pamoja na mke wake walikuwa wanatafutwa na polisi kwa kipindi cha mda mrefu kufuatia kuhusika na matukio mbalimbali ya uhalifu  ,mauaji pamoja na  wizi ambao ulishawahi kutokea jijini hapa .

Hata hivyo Sabas alisema kuwa Katika tukio lingine  mwanamke mmoja ambaye amefahamika kwa jina la Konsolata Tarimo (30)mkazi wa ngaramtoni amekamatwa na jeshi la polisi akiwa na risasi  46 za bunduki aina ya smg  pamoja na vifaa mbalimbali za bunduki hiyo ikiwemo  kifaa cha kusafishia silaha hiyo.

Alibainisha kuwa mwanamke huyo alikutwa nyumbani kwake majira ya saa nane usiku kuamkia September 6 wakati askari waliokuwa doria walipofanya msako wa kushutukiza Katika nyumba hiyo  baada ya kutilia shaka.

Alisema kuwa askari hao walipofanya msako huo  walikuta risasi hizo 46 za bunduki hiyo aina ya smg  ,muhuri ambao ulikuwa umeandikwa pande zote mbili huku pande ya kwanza ikiwa imeandikwa District game office simanjiro na upande mungine umeandikwa district game of monduli district,kifaa cha kubusti risasi Katika bunduki hiyo ya smg pamoja na kifaa cha kusafishia silaha hiyo inayotumiwa na risasi hizo.

Aidha alibainisha kuwa silaha ambayo ilikuwa inatumika kwa ajili ya silaha hiyo haijakamatwa bali msako mkali unaendelea ili kukamata silaha hiyo iliyokuwa ikitumia risasi hizo.

Alisema kuwa watuhumiwa wote bado wapo chini ya ulinzi  kwa ajili yamahojiano  na pindi upelelezi utakapo kamilika watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo.

Wakati huo huo Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina Ibrahimu Saloni(30) mkazi wa sakina amefariki dunia mara baada ya kugongwa na gari aina hince na kupoteza maisha  papo hapo

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kamanda wa polisi Mkoani hapa alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa kumi jioni katika barabara ya makao mapya mtaa wa levolosi jijiji hapa .

Alisema kuwa mtu  dereva wa gari hilo aina ya hince  yenye namba za usajili T225 BZE alitambulika kwa jina la Shaban Mohamed (27)mkazi wa tengeru.

Alisema kuwa gari hilo lilikuwa likitokea barabara kuu  kuelekea barabara ya kati makutano ndipo dereva hoyo alimgonga mwendesha  baskeli

Shuhuda wa Ajali hiyo Bi.Ashura Ali ambaye shughuli zake ni mamantilie alisema kuwa hiyo ni mara ya pili kwa ajali kutoke katika eneo hilo na huku wanaogogwa kupoteza maisha kutokana na mwendo kasi wa madereva 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Wananchi wenye hasira kali wamemtupia lawama mkandarasi anayeshughulikia barabara zote za katikati ya Mji wa Arusha hususani brabara ya kati makutano mtaa wa Levolosi kwa kutoweka matuta wala alama za barabarani yanayodhibi mwendo kasi hali inayopelekea ajali za mara kwa mara kutokea huku Viongozi husika wakifumbia macho.

No comments:

Post a Comment