Kamanda
wa polisi Mkoa wa Arusha Bw.Liberatus Sabas akiwa anawaonyesha
waandishi wa habari risasi,pisto na kifaa cha kunyooshea risasi jana
ofisini kwake.
Wanachi wakiwa wanaangalia mwili wa marehemu mara baada ya kugongwa na gari jana katika barabara ya katimakutano jijini Arusha
Mahmoud Ahmad,Arusha
Jeshi
la polisi mkoani Arusha limefanikiwa kuwakamata majambazi sugu watatu
kwa nyakatitofauti wakiwa na silaha aina ya pisto yenye risasi tano
pamoja na mashine ya kunyooshea bunduki , kifaa cha kubustia risasi
pamoja na risasi 46 za bunduki aina ya smg Katika matukio mawili
tofauti.
Akiongea
na waandishi wa habari mkoani hapa kamanda wa polisi mkoa wa Arusha
Liberatus Sabas alisema kuwa matukio hayo mawili yalitokea kwa nyakati
tofauti Katika maeneo tofauti ya mkoani hapa kufuatia msako mkali
uliokuwa ukifanya na jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi
wasamaria wema.
Kamanda
alisema kuwa Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa ni jambazi sugu
aliyejihusisha na matukoi ya hivi karibuni aliyefahamika kwa jina la
Salimu Kiwele alimaarufu kwa jina la Msaula(39)mkazi wa sombetini mkoani
hapa akiwa na mke wake aliyetambulika kwa jina la Princes Juma (34)
wote ni wakazi wa sombetini wamekamatwa nyumbani kwao wakiwa na silaha
pamoja na risasi.
Alisema
kuwa watu hao walikamatwa wakiwa na silaha aina ya pisto Glock FFN 350
ikiwa na risasi tano ambazo zilikuwa ndani ya magazine ya silaha hiyo.
Alisema
kuwa mtu huyu pamoja na mke wake walikuwa wanatafutwa na polisi kwa
kipindi cha mda mrefu kufuatia kuhusika na matukio mbalimbali ya uhalifu
,mauaji pamoja na wizi ambao ulishawahi kutokea jijini hapa .
Hata
hivyo Sabas alisema kuwa Katika tukio lingine mwanamke mmoja ambaye
amefahamika kwa jina la Konsolata Tarimo (30)mkazi wa ngaramtoni
amekamatwa na jeshi la polisi akiwa na risasi 46 za bunduki aina ya
smg pamoja na vifaa mbalimbali za bunduki hiyo ikiwemo kifaa cha
kusafishia silaha hiyo.
Alibainisha
kuwa mwanamke huyo alikutwa nyumbani kwake majira ya saa nane usiku
kuamkia September 6 wakati askari waliokuwa doria walipofanya msako wa
kushutukiza Katika nyumba hiyo baada ya kutilia shaka.
Alisema
kuwa askari hao walipofanya msako huo walikuta risasi hizo 46 za
bunduki hiyo aina ya smg ,muhuri ambao ulikuwa umeandikwa pande zote
mbili huku pande ya kwanza ikiwa imeandikwa District game office
simanjiro na upande mungine umeandikwa district game of monduli
district,kifaa cha kubusti risasi Katika bunduki hiyo ya smg pamoja na
kifaa cha kusafishia silaha hiyo inayotumiwa na risasi hizo.
Aidha
alibainisha kuwa silaha ambayo ilikuwa inatumika kwa ajili ya silaha
hiyo haijakamatwa bali msako mkali unaendelea ili kukamata silaha hiyo
iliyokuwa ikitumia risasi hizo.
Alisema
kuwa watuhumiwa wote bado wapo chini ya ulinzi kwa ajili yamahojiano
na pindi upelelezi utakapo kamilika watafikishwa mahakamani haraka
iwezekanavyo.
Wakati
huo huo Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina Ibrahimu Saloni(30) mkazi wa
sakina amefariki dunia mara baada ya kugongwa na gari aina hince na
kupoteza maisha papo hapo
Akithibitisha
kutokea kwa ajali hiyo kamanda wa polisi Mkoani hapa alisema kuwa tukio
hilo lilitokea majira ya saa kumi jioni katika barabara ya makao mapya
mtaa wa levolosi jijiji hapa .
Alisema kuwa mtu dereva wa gari hilo aina ya hince yenye namba za usajili T225 BZE alitambulika kwa jina la Shaban Mohamed (27)mkazi wa tengeru.
Alisema kuwa mtu dereva wa gari hilo aina ya hince yenye namba za usajili T225 BZE alitambulika kwa jina la Shaban Mohamed (27)mkazi wa tengeru.
Alisema kuwa gari hilo lilikuwa likitokea barabara kuu kuelekea barabara ya kati makutano ndipo dereva hoyo alimgonga mwendesha baskeli
Shuhuda
wa Ajali hiyo Bi.Ashura Ali ambaye shughuli zake ni mamantilie alisema
kuwa hiyo ni mara ya pili kwa ajali kutoke katika eneo hilo na huku
wanaogogwa kupoteza maisha kutokana na mwendo kasi wa madereva
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti Wananchi wenye hasira kali wamemtupia lawama
mkandarasi anayeshughulikia barabara zote za katikati ya Mji wa Arusha
hususani brabara ya kati makutano mtaa wa Levolosi kwa kutoweka matuta
wala alama za barabarani yanayodhibi mwendo kasi hali inayopelekea ajali
za mara kwa mara kutokea huku Viongozi husika wakifumbia macho.
No comments:
Post a Comment