Mkuu
wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi akizungumza wakati wa semina ya
waandishi wa habari ambapo pamoja na mambo mengine amezungumzia swala la
kuweka jiji katika hali ya usafi akisema kuwa Manispaa ya Ilala
inakusudia kuingia ubia na wanahabari katika kufanikisha lengo la kuwa
Manispaa safi ukizingatia ndio kitovu cha mji wa Dar es Salaam.
Ametumia
nafasi hiyo kuwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika kugharamia
usombaji wa taka kwani wengi wao wamekuwa wakiona gharama wanazotozwa
kwa ajili ya kubeba taka ni kubwa lakini watambue kuwa kwa siku taka
zinazokusanywa hufikia hadi tani 1088.
Baadhi
ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini wakimsikiliza
kwa makini mkuu wa wilaya ya Ilala wakati akizungumzia mikakati ya
Manispaa hiyo kuhakikisha inakuwa mfano wa kuigwa kwa usafi jijini.
Pichani Juu na Chini ni baadhi ya waandishi wa habari wakichangia maoni yao namna ya kuboresha Usafi katika Manispaa hiyo.
Afisa
Usafishaji wa Manispaa ya Ilala Bw. Samuel Bubegwa akitoa Elimu kwa
wanasemina kuhusiana na jinsi Manispaa hiyo inavyotumia mbinu mbadala
baada ya kukusanya taka ambapo huzichambua na kuziweka katika makundi
tofauti na nyingine kutumika kuzalishia mbolea ambayo inauzwa na kukuza
kipato cha kuendeshea huduma mbalimbali ndani ya manispaa hiyo.
Mwanasheria
wa Manispaa ya Ilala Bi. Pamela Mugaruka akielezea matumizi ya sheria
ndogo ambazo zimetungwa mwaka 2011 kwa watu wanaozikiuka wakiwemo
wanaogoma kulipa ada na kufafanua makosa, adhabu ikiwemo faini
zitakazowakabili kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha sheria hizo.
Mwenyekiti
wa Kata ya Mwenbe Madafu Wifred Kipondya akielezea mafanikio
yaliyofikwa na kata yake kutokana na utaratibu waliojiwekea wa kukusanya
kodi ambapo sasa wameweza kufikia kukusanya hadi shilingi Milioni 70.
Chati
ya mapato na matumizi kwa mwezi kwa mwaka 2009 iliyowasilishwa
na Mwenyekiti wa Kata ya Mwembe Madafu Bw. Wifred Kipondya iliyopo ndani
ya Manispaa ya Ilala wakati wa semina ya waandishi wa habari.
Baadhi ya maafisa wa Manispaa ya Ilala na waandishi wa habari waliohudhuria semina hiyo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment