Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
-----
NA MWANDISHI WETU, MWANZA
Katibu
wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, amesema
dalili za kubwagwa kwa CHADEMA ndizo zilizomkimbiza mapema jijini
Mwanza, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willbroard Slaa.
Amesema
kushindwa kwa Chadema katika kinyang’anyiro cha Meya na Naibu Meya, ni
mavuno ya ubabe wa viongozi wa chama hicho ambao baadhi wanazeeka
vibaya.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa,
Nape (pichani) alisema kwamba, Slaa alikimbia baada ya kuona maji
yamezidi unga.
Nape
aliyetumia fursa hiyo pia kuwapongeza Madiwani wa CCM wa wilaya ya
Nyamagana na Chama kwa ushindi wa Viti vya Meya na Naibu wake, alisema
Dk. Slaa anazeeka viba ndiyo maana naongoza chama hicho kwa ubabe na
maandamano ya kila mara.
“Babu
(akiwa na maana ya Dk Slaa) alisema CCM Mwanza itaondoka madarakani,
imejidhihirisha wazi katika uchaguzi wa leo kuwa CCM bado ina nguvu na
ni Chama kikongwe kisiasa, vingine vinaiga.”
“Chadema
wameona mavuno ya ubabe wao japo kura za CCM ni ndogo…., Babu ajiulize
kwa nini ameshindwa kwenye uchaguzi huo wa Meya na Naibu Meya.” Alisem
Nape na kuongeza kwamba, kutokana na dalili za kushindwa zilizoonekana
mapema, ndiyo maana Dk Slaa alikimbia Mwanza mapema.
Akiwapongeza
madiwani hao kwa ushindi alisema kwamba wamefanya kazi kubwa na ya
ziada kuhakikisha CCM inarejesha Halmashauri ya jiji hilo mikononi mwake
baada ya kushikwa na Chadema kwa kipindi kifupi na hivyo kuwataka wana
Mwanza wawe na mshikamano na kuwapa ushirikiano viuongozi wao.
“Nawasihi
wananchi wa Mwanza wawe na mshikamano na kuacha maandamano yasiyokuwa
na msingi, badala yake wafanye maandeleo, waimamini CCM sasa inachokuja
kufanya ni cha uhakika.” Alieleza Nape.
No comments:
Post a Comment