……………………………………………..
ALIYEKUWA muasisi wa Chama cha
Mageuzi ya Kitaifa (NCCR-Mageuzi), Emmanuel Petro Ole Sirikwa amefariki
dunia juzi kwenye hospitali ya AICC jijini Arusha alikokuwa amelazwa
akisumbuliwa na maradhi ya kiharusi.
Akizungumza na wandishi wa habari
kwenye ofisi za Chama hicho jijini Dar es Salaam jana Naibu Katibu Mkuu
kwa upande wa Zanzibar, Mussa Kombo Mussa, alisema chama kimepoteza
mwanamageuzi wa kweli katika ulingo wa siasa nchini.
“Chama kimempoteza mtu muhimu,
alikuwa ndiye kinara alikuwa miongoni mwa wanchama mwenye kadi Na. 3 za
mwanzo kwani waliokuwa na kadi Na.1 na Na. 2, ni wale waliyojiingiza
kwenye misuko suko ya kijamii, kisiasa na kiuchumi iliwafanya wamsaliti
mtoto waliyemzaa (NCCR-Mageuzi) na kukimbilia vyama vingine”alisema
Mussa.
Mussa alisema Ole Sirikwa
alifariki usiku wa kuamkia Oktoba 28 mwaka huu katika hospitali hiyo,
ambako alilazwa kwa majuma mawili baada ya kuugua ugonjwa huo kwa muda
mfupi.
Akifafanua kuhusu nyadhifa
alizoshika ndani ya chama hadi alipofikwa na mauti, Naibu Katibu Mkuu
huyo, alisema Ole -Sirikwa alikuwa Kamishna wa chama, Mkoani Arusha, na
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa pia Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la
chama. Alikuwa mmoja wa waanzilishi wa NCCR – Mageuzi akiwa anamiliki
kadi namba 03 ya uanachama.
Nafasi nyingine za uongozi
alizowahi kuwa nazo ni pamoja Mwenyekiti wa Mkoa na mjumbe wa Kamati Kuu
ya Taifa (kabla ya mabadiliko ya Katiba).
“Kutokana na heshima na historia
yake ndani ya chama, na vilevile ikizingatiwa kuwa mapenzi ya Mwenyezi
Mungu hayana makosa na wala hayawezi kukatiwa rufaa. Chama kimeamua
kuenzi uvumilivu na misimamo yake kwa kuuita ukumbi wa mikutano wa chama
chetu kwa jina la Ukumbi wa Sirikwa”alisema
Mussa alisema M\maziko yanatarajiwa kufanyika Kijijini kwake Olijilah- Arumeru Mkoani Arusha Oktoba 3mwaka huu.
Katika maziko hayo, chama
kitawakilishwa na viongozi wakuu wa chama wakiongozwa na Ndugu James
Francis Mbatia (Mb), Mwenyekiti wan Chama Taifa.
Marehemu amefariki akiwa na umri wa miaka 70, pia ameacha mjane na watoto watatu.
No comments:
Post a Comment