Pages

Sunday, September 30, 2012

MUASISI WA CHAMA CHA NCCR MAGEUZI AFARIKI DUNIA ARUSHA



Naibu Katibu Mkuu kwa upande wa Zanzibar, Mussa Kombo Mussa
……………………………………………..
ALIYEKUWA muasisi wa Chama cha Mageuzi ya Kitaifa (NCCR-Mageuzi), Emmanuel Petro Ole Sirikwa amefariki dunia juzi kwenye hospitali ya AICC jijini Arusha  alikokuwa amelazwa akisumbuliwa na maradhi ya kiharusi.
 
Akizungumza na wandishi wa habari kwenye ofisi za Chama hicho jijini Dar es Salaam jana Naibu Katibu Mkuu kwa upande wa Zanzibar, Mussa Kombo Mussa, alisema chama kimepoteza mwanamageuzi wa kweli katika ulingo wa siasa nchini.
“Chama kimempoteza mtu muhimu, alikuwa ndiye kinara alikuwa miongoni mwa wanchama mwenye kadi  Na. 3 za mwanzo kwani waliokuwa na kadi Na.1 na Na. 2,  ni wale waliyojiingiza kwenye misuko suko ya kijamii, kisiasa na kiuchumi  iliwafanya wamsaliti mtoto waliyemzaa (NCCR-Mageuzi) na kukimbilia vyama vingine”alisema Mussa.
 
Mussa alisema  Ole Sirikwa alifariki usiku wa kuamkia Oktoba 28 mwaka huu katika hospitali  hiyo, ambako  alilazwa kwa majuma mawili baada ya kuugua ugonjwa huo kwa muda mfupi.
Akifafanua kuhusu nyadhifa alizoshika ndani ya chama hadi alipofikwa na mauti, Naibu Katibu Mkuu huyo, alisema Ole -Sirikwa alikuwa Kamishna wa chama, Mkoani Arusha, na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa pia Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la chama. Alikuwa mmoja wa waanzilishi wa NCCR – Mageuzi akiwa anamiliki kadi namba 03 ya uanachama.
Nafasi nyingine za uongozi alizowahi kuwa nazo ni pamoja Mwenyekiti wa Mkoa na mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa (kabla ya mabadiliko ya Katiba).
 
“Kutokana na heshima na historia yake ndani ya chama, na vilevile ikizingatiwa kuwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu hayana makosa na wala hayawezi kukatiwa rufaa. Chama kimeamua kuenzi uvumilivu na misimamo yake kwa kuuita ukumbi wa mikutano wa chama chetu kwa jina la Ukumbi wa Sirikwa”alisema
Mussa alisema M\maziko yanatarajiwa kufanyika Kijijini kwake Olijilah- Arumeru Mkoani Arusha Oktoba 3mwaka huu.
Katika maziko hayo, chama kitawakilishwa na viongozi wakuu wa chama wakiongozwa  na Ndugu James Francis Mbatia (Mb), Mwenyekiti wan Chama Taifa.
 Marehemu amefariki akiwa na umri wa miaka 70, pia  ameacha mjane na watoto watatu.

No comments:

Post a Comment