Pages

Sunday, September 30, 2012

NIZAR AING'ARISHA YANGA AKITOKEA BENCHI, SALAMU ZAO SIMBA ZENJI




YANGA imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya African Lyon katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Shukrani kwake kiungo anayecheza kwa nadra kwenye timu hiyo, Nizar Khalfan aliyefunga mabao ya ushindi dakika ya 65 na 88, akitokea benchi kuchukua nafasi ya Frank Domayo.
Nizar alifunga bao la pili, sekunde chache baada ya Benedictor Mwamlangala kuisawazishia African Lyon bao lililodumu tangu dakika ya 17, baada ya Nahodha wa Yanga, kutangulia kufunga dakika ya 17.
Ushindi huo, unaifanya Yanga ifikishe pointi saba, baada ya kucheza mechi nne na kupanda hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi, ikiwa inalingana na Coastal kwa pointi na wastani wa mabao, ingawa Coastal wako nyuma kwa mechi moja.
Simba bado inaongoza ligi hiyo, kwa pointi zake 12, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 10.  
Yanga SC; Ally Mustapha 'Barthez', Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Kevin Yondan, Nadir Haroub 'Cannavaro', Athumani Iddi 'Chuji',  Simon Msuva, Frank Domayo/Nizar Khalfan, Didier Kavumbagu, Hamisi Kiiza/Said Bahanuzi na Haruna Niyonzima.

Didie Kavumbagu wa Yanga (Kushoto),ibu kumtoka mlinzi wa African Lyon, kwenyepambano la soka ligi kuu ya Tanzania bara kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam yanga imeshinda bao tatu kwa moja 3-1leo mabao yamefungwa na Nadir harub kanavalo bao moja na Nizaa Khalfan amefunga mabao 2 


Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva, (Kulia), akitafuta mbinu za kumtoka mlinzi wa Afrikan Lyon, Sunday Bakari katika pambano la ligi kuu soka Tanzania bara kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam yanga imeshinda bao 3-1 leo
PICHA KWA HISANI YA MZUKA WA FUNGO

No comments:

Post a Comment