Brandts wa pili kutoka kulia, akiwa na viongozi wa Yanga. Kulia ni Seif Magari. Kushoto kwake ni Bin Kleb na Majjid |
Anapakia mizigo kwenye gari la Bin Kleb |
Anazungumza na Waandishi wa Habari |
Akiwa na viongozi wa Yanga |
Kulia kwake Bin Klerb, kushoto Mwalusako |
Anatoka Uwanja wa Ndege |
KOCHA mpya wa Yanga, Ernstus ‘Ernie’ Wilhelmus Johannes Brandts, beki wa zamani
wa kimataifa wa Uholanzi na klabu ya PSV Eindhoven ya Holanzi, amewasili Jana
usiku (saa 3:45) katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere
na ndege ya KLM tayari kusaini mkataba na kuanza kazi katika klabu hiyo.
Brandts amepokewa na Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako na viongozi
wengine,
Abdallah Ahmad Bin Kleb, Seif Ahmad ‘Magari’ na Majjid Suleiman na
amesema anaijua Yanga ni timu nzuri, kubwa hana shaka ataiwezesha
kufanya vizuri katika
medani ya soka Afrika.
Yanga, imetimiza malengo yake ya kuwa kocha mpya, kabla ya kucheza na wapinzani
wao
wa jadi, Simba SC, Oktoba 3, mwaka huu baada ya kumfukuza Mbelgiji, Tom
Saintfiet, kutokana na kuwasili makubaliano na Brandts, ambaye ataanza
kazi mara moja kesho.
Mholanzi huyo aliyefukuzwa APR ya Rwanda baada ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki
na Kati, Kombe la Kagame, Agosti mwaka huu amepewa ukocha wa Yanga, baada ya
Mbrazil Marcio Maximo kukataa nafasi hiyo kwa mara ya pili.
Mtaalamu huyo, alizaliwa Februari 3, mwaka 1956 mjini Nieuw-Dijk, Gelderland, mbali
na PSV Eindhoven, alichezea pia Roda JC Kerkrade, MVV Maastricht na De Graafschap.
Brandts aliichezea mechi 28 timu ya taifa ya Uholanzi na kuifungia mabao matano na
pia alicheza Fainali za Kombe la Dunia mwaka 1978.
Katika fainali hizo, Raundi ya pili kwenye mechi na Italia, aliweka rekodi ya kuwa
mchezaji pekee aliyezifungia mabao timu zote katika mechi moja kwenye fainali za
Kombe la Dunia.
Alianza kujifunga dakika ya 18, kisha akaisawazishia Uholanzi dakika ya 50 katika
mechi ambayo, mchezaji mwenzake Arie Haan baadaye aliifungia timu yake bao la
ushindi na kutoka kifua mbele kwa mabao 2–1.
Alipostaafu
soka akawa kocha na katikati ya msimu wa 2007–2008, Brandts aliambiwa
hataongezewa mkataba NAC-Breda, licha ya matokeo mazuri ya kushika
nafasi ya tatu
katika Ligi Kuu Uholanzi (Eredivisie), ingawa uamuzi huo haukuwafurahisha
mashabiki wa timu hiyo na nafasi yake akapewa Robert Maaskant kuanzia
msimu wa 2008–2009.
Akateuliwa kuwa Kocha wa Rah Ahan mwaka 2009, kabla ya kufukuzwa Desemba
2009 na kuibukia APR ya Rwanda mwaka 2010, ambako ‘riziki’ yake imeisha miezi
miwili iliyopita na sasa amepata maisha mapya Yanga.
Akiwa APR, Brandts alifungwa mechi zote mbili na Yanga iliyokuwa ikifundishwa
na Mbelgiji Tom Saintfiet katika Kombe la Kagame, moja ya makundi 2-0 na nyingine
ya Nusu Fainali 1-0. Yanga iliibuka bingwa, ikiifunga Azam FC 2-0 kwenye fainali.
Brandts atakutana na wachezaji wake wa zamani wawili Yanga, beki Mbuyu Twite
anayeanza msimu wa kwanza katika klabu hiyo na kiungo Haruna Niyonzima
anayeingia katika msimu wa pili, ambao alifanya nao kazi APR. source bin zubeiry
No comments:
Post a Comment