Pages

Thursday, September 27, 2012

RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AFUNGUA SEMINA YA VIONGOZI WA KISIASA ZANZIBAR



 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akifungua Semina ya tatu ya kuimarisha Uhusiano Baina ya Viongozi wa Kisiasa na Kiutendaji katika Serikali za Mitaa Zanzibar, katika ukumbi wa Misali Sunset Beach Hotel Wesha Pemba. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu
 Mwakilishi wa Shirika la UNDP mjini Zanzibar, Njeri Kamau, akiwasilisha salamu za Shirika hilo katika Semina ya siku tatu ya Uimarishaji uhusiano baina ya Viongozi wa kisiasa na Kiutendaji katika Serikali za Mitaa, iliyoanza leo katika ukumbi wa Misali sunset Beach Hotel Wesha Pemba.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Mwinyihaji makame Mwadini akitoa nasahha zake na kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein,kuifungua Semina ya siku tatu kuhusu Uimarishaji Uhusiano baina ya Viongozi wa kisiasa na Kiutendaji katika Serikali za Mitaa,katika ukumbi wa Misali Sunset Beach Hotel Wesha Pemba leo.
Baadhi ya Madiwani na Masheha wa Shehia mbali mbali za Pemba,wakiwa katika Semina ya siku tatu Kuhusu Uimarishaji uhusiano baina ya Viongozi wa Kisiasa na Kiutendaji katika Serikali za Mitaa,iliyoanza leo,chini ya  Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,  katika Ukumbi Misali Sunset Beach Hotel Wesha Pemba.

No comments:

Post a Comment