Mkurugenzi
wa Kamati ya Miss Tanzania Bw. Hashim Lundega akiongea na waandishi wa
habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo kuhusu shindano hilo
kulia ni Meneja wa bia ya Redds na kushoto ni Miss Tanzania 2011 Salha
Israel.
Mashindano
ya Redds Miss Tanzania kwa sasa yamekamilika katika hatua zote na hatua
ya mwisho ilikuwa hatua ya kanda ambayo kwa sasa imekamilika na
kufanikiwa kuwapa warembo jumla ya 30 .endelea kupitia audifacejackson
blogspot kujua kila linalojiri kila saa duniani kote..Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam Mkurugenzi wa LINO AGENCY
Hashim Lundenga alisema mashindano kiujumla katika ngazi zote hadi kanda
yamekuwa na mafanikio makubwa na kuonyesha kuwa fainali ya Taifa ya
mwaka huu itakuwa na ushindani wa hali ya Juu.
Washiriki
wengi wa mwaka huu kwa asilmia 90 ni wasomi wanafunzi wa Vyuo Vikuu
na wengine wanatarajia kujiunga na Vyuo Vikuu, jambo ambalo litaleta
hamasa kubwa katika shindano la mwaka huu.
Baada
ya kukamilika kwa mashindano hayo ya Kanda kwa sasa tunatangaza rasmi
kuwa warembo wote 30 walioshinda na kuingia katika kinyang,anyiro cha
Redds Miss Tanzania 2012 wataingia kambini siku ya jumanne October
2,2012 katika Hotel yenye hadhi ya kitalii ya GIRAFFE HOTEL Iliyopo
hapa Jijini Dar Es salaam,Washiriki hao watakuwa kambini kwa muda wa
mwezi mmoja.
Tunapenda
kuwajulisha wadau wa tasnia ya urembo kwamba shindano la REDDS MISS
TANZANIA 2012 litafanyika siku ya Jumamosi tarehe 03 November 2012
katika Ukumbi wa Hotel ya Blue Peal (Ubungo Plaza).
Kwa
Upande wake Meneja wa Kinywaji cha Redds Original Victoria Kimaro
alisema wao kama wadhamini wakuu wa Redds Miss Tanzania wamejipanga kwa
nguvu kubwa kutoa burudani ya aina yake kwa wadau wote wa tasnia ya
urembo hapa nchini sambamba na kuhakikisha warembo wote waliofanikiwa
kuingia hatua ya fainali watapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali.
Kwa
kuzingatia mabadiliko ya Kalenda ya Mashindano ya urembo ya Dunia,
Mrembo wa Tanzania atakuwa na muda mrefu wa maandalizi kwani atatakiwa
kuripoti katika Fainali za Mashindano ya urembo ya Dunia katikati ya
mwaka ujao. 2013.
No comments:
Post a Comment