Mhariri
Mtendaji wa kampuni ya Free Media Ltd. Absalom kibanda akizungumza kwa
uchungu wakati wa kumuaga aliyekuwa mfanyakazi wa kampuni hiyo Bi. Agnes
Yamo ambapo pamoja na kutangaza kugharamia msiba huo pia amesema tasnia
ya habari imepoteza mtu mahiri aliyekuwa na upeo.
Katibu
wa Jukwaa la Wahariri Neville Meena akielezea jinsi jukwaa hilo
lilivyopokea kwa masikitiko taarifa za kufariki kwa Bi. Agnes Yamo na
kuwa wataendelea kumkumbuka kwa kazi zake za kiuandishi.
Mwakilishi
wa Jeshi la Polisi Kitengo cha Usamala barabarani akizungumza wakati wa
kuuaga mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari wa Kampuni ya Tanzania
Daima.
Mhariri
Mtendaji wa kampuni ya Free Media Ltd wanaomiliki gazeti ya Tanzania
Daima Absolum Kibanda amesema marehemu Agned Yamo alitumua muda wake
kuwaasa kuomba kwa ajili yake.
Kibanda
amesema hayo wakati wa kutoa salamu za mwisho kwa marehemu Agnes ambaye
alifariki juzi asubuhi kwenye hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam.
Awali
salamu mbalimbali zilitolewa zikiwemo kutoka kwa Jukwaa la Wahariri
ambapo Katibu wa Jukwaa hilo Bw. Nevile Meena amesema Jukwaa limepoteza
mwandishi kijana.
Meena
amesema anatufundusha kuwa na mahusiano mema na watu wengi, na pia
ametumia fursa hiyo kuwapa pole familia yake na kuongeza kuwa wanaamini
Mungu aliyemleta kwa miaka 34 iliyopita ataleta mwingine.
Hata
hivyo Kampuni hiyo imegharamia shughuli zote za msiba huku Mtandao wa
Waandishi wa Habari ulitoa kiasi cha fedha kama rambirambi.
Aidha Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama kilitoa ubani kwa ajili ya msiba huo.
No comments:
Post a Comment