Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, September 28, 2012

STR8MUZIK Free Style 2012 zang’ara Mwanza


Mmoja wa wanakundi cha waburudishaji cha BFB cha mkoani Mwanza akifanya vitu vyake katika mpambano wa kusaka ma-MCs na DJs wa STR8MUZIK Freestyle 2012 mkoani Mwanza uliofanyika katika ukumbi wa Stone mjini humo jana usiku.
Msanii wa kizazi kipya Easy Business ambaye ni maarufu kwa kibao chake cha “Ongea na Mshua” akitumbuiza katika mpabano wa STR8MUZIK 2012 FreeStyle Mwanza.
Mashabiki wa ST8MUZIK Freestyle 2012 mkoani Mwanza wakiwa wamembeba juu MC bora wa mwaka mkoani humo Joash Magadula katika mpambano uliofanyika jana usiku katika ukumbi wa Stone mjini humo.
Umati wa wana-Mwanza ulivyoshona katika ukumbi Club Stone mjini humo katika mpambano wa STR8MUZIK 2012 FreeStyle Mwanza.
Mshindi wa mpambano wa ma-DJ wa ST8MUZIK Freestyle 2012 mkoani mwanza DJ Juma Ramadhani(Kati) akitumbuiza mara baada ya kukabidhiwa chombo cha kupigishia muziki chenye thmani ya Sh mil 7 na Meneja wa TCC Mkoa wa Mwanza Deogratius Kamugisha(Kulia), huku mshindi wa upande wa ma-MC mkoani humo Joash Magadula akishuhudia na zawadi yake mkononi.
Meneja wa TCC Mkoani Mwanza Deogratius Kamugisha akimkabidhi tuzo MC bora wa ST8MUZIK Freestyle 2012 mkoani Mwanza Joash Magadula katika mpambano uliofanyika katika ukumbi wa Stone mjini humo jana.
Meneja wa TCC tawi la Mwanza, Bw Deogratius Kamugisha (Katikati) akipozi na washindi wa mpambano wa ma MCs na DJs STR8MUZIK Freetyle 2012 mkoani mwanza. Kutoka kushoto ni Mshindi wa pili wa DJs Ruyobya Johannes a.k.a DJ Yt,Mshindi wa kwanza kwa DJs Juma Ramadhani,Msindi wa Pili katika kategori ya ma-MCs Nchana Antony na Mshindi wa MCs Joash Magadula a.k.a MC Magadash.
*****************************************
Na Mwandishi wetu Mwanza

FAINALI za tamasha la muziki la  STR8  zilimalizika jana mjini hapa kwa kishindo cha aina yake huku tuzo ya DJ bora yenye thamani ya thamani ya sh milioni saba ikimuangukia DJ Juma Ramadhani.

Ilikuwa ni patashika nguo kuchanika wakati ma DJs na Ma MCs wakipambana vikali kuwania moja ya kifaa cha kisasa kabisa katika masuala ya kuchezesha muziki, DJ Pioneer.

Ruyobya Johaness a.k.a DJ YT alikamata nafasi ya pili katika kategori ya MCs akiondoka zawadi kadhaa  zikiwemo fedha taslimu 100,000/= .

Mshindi katika kategori ya MC  alikuwa ni Joash Magadula ambaye pamoja na tuzo pia amepata nafasi ya kurekodi albamu katika moja ya studio tatu  bomba za muziki nchini.

Nchana Anthony, alishika nafasi  ya pili katika kategori hiyo ya ma-MC aliondoka nyumbani na zawadi kadhaa na fedha taslimu  100,000/=.

Fainali hizo ambazo ni za tatu tangu zianzishwe nchini zinaratibiwa na  kampuni ya Sigara nchini (TCC) kwa lengo la kukuza vipaji miongoni mwa vijana na kutengeneza nafasi ya ajira.

Michuano hiyo ambayo ilikuwa na  maMc 85 na Madj 25 zilichuja washindani wake hadi 16 kwa MC na  10  kwa maDJ katika raundi ya kwanza kabla ya raundi ya pili kutoa washiriki wa fainali.

Wakati MaDJ wakichukua nafasi zao katika tamasha hilo wapenzi wa burudani hawakuwa na la kufanya zaidi ya kuondoka na staili zao huku wakiwafagilia au kuwazodoa hivyo kuwapanga kimtindo katika nafasi za ushindani .

MaDJ hao  walipewa maksi kwa kuangaliwa na majaji kuhusu uwezo wao wa kuchanganya muziki, uwezo wa kiufundi na wanavyomudu vifaa wanavyofanyiakazi na jinsi wanavyoburudisha.

Ma DJ sita waliofika fainali walikuwa Bernard Fabian, DJ Yt, Robert Rowan, DJ Megastar, Tony Wyclif na Juma Ramadhani.

Kategori ya MC  ilihusisha  DJ kupewa mada ya kukieleza kwa mtindo wa kufoka foka kwa dakika tatu kiushairi kimpangilio.

Raundi ya kwanza ya kategori hiyo ilihusisha MCs wote kisha ikawapunguza kwa pea hali ambayo ilifanya fainali hizo kuwa burudani babu kubwa hasa kutokana na jinsi  wahusika walivyowachambua wenzao.

Matukio hayo ya fainali yalinogeshwa na burudani mbalimbali zikiwamo zilizotolewa na wakali wa Bongo Fleva kama Easy Business ambaye anajulikana kitaani kwa wimbo wake wa  ‘Ridhiwani Ongea na Mshua’ .

Pia walikuwapo vijana wa kundi la Mwanza la BFB ambapo madansa wake walivamia jukwaa kwa staili huru zilizowapeleka puta  wapenzi wa burudani waliokuwapo hapo.Madansa hao waliondoka  kwa mitindo tofauti ikiwamo ya sarakasi na pop.

Aliyetingisha zaidi katika  vionjo ni yule aliyetwaa ushindi mwaka 2010 katika kategori ya MCs, DJ Simba, ambaye alionesha ubabe wake katika kucheza na biti kiasi cha kufanya  ukumbi mzima kurindima kwa shangwe.

Katika kategori ya  MCs majaji waliangalia uwezo wa washiriki katika kumiliki maikrofoni,ufundi wake, uhalisia na staili.

Kwa mujibu wa waratibu wa michuano hiyo, ilikuwa taabu kubwa kumpata mshindi kutokana na wahusika kuwa wakali katika nafasi zao hali inayodhirisha utajiri wa vipaji vya muziki miongoni mwa vijana.

“Viopaji hivi vinatakiwa kulelewa na kuendelezwa,” alisema Deogratius Kamugisha, mwenyeji wa mashindano haya ambaye pia ni Meneja wa TCC Mwanza.

Alisema kwamba michuano hiyo ilikuwa si tu burudani bali pia ilitoa mwanya wa mafanikio mengine kama ajira.

Alisema washindi wa michuano iliyopita kwa sasa wako katika ajira mbalimbali zikiwemo vilabu vya usiku na vituo vya radio.

Kamugisha  aliongeza: ” Hii ni namna ya kutengeneza ajira” alisema na kuongeza kwamba mashine ya kuchezea muziki kama aliyopewa Juma Ramadhani ni chanzo cha ajira  kwani anaweza kuitumia yeye au kuikodisha kwa wengine anapokuwa hana kazi nayo.

Mchuano mingine miwili itafanyika mjini Dar es Salaam na Mbeya kukamilisha tamasha la mwaka huu.(Picha zote na Executive Solutions)

No comments:

Post a Comment