Pages

Wednesday, September 26, 2012

WANAHABARI WAMUAGA MWENZAO AGNES YAMO LUGALO JIJINI DAR.



Mhariri Mtendaji wa kampuni ya Free Media Ltd. Absalom kibanda akizungumza kwa uchungu wakati wa kumuaga aliyekuwa mfanyakazi wa kampuni hiyo Bi. Agnes Yamo ambapo pamoja na kutangaza kugharamia msiba huo pia amesema tasnia ya habari imepoteza mtu mahiri aliyekuwa na upeo.
 Katibu wa Jukwaa la Wahariri Neville Meena akielezea jinsi jukwaa hilo lilivyopokea kwa masikitiko taarifa za kufariki kwa Bi. Agnes Yamo na kuwa wataendelea kumkumbuka kwa kazi zake za kiuandishi.
Mwakilishi wa Jeshi la Polisi Kitengo cha Usamala barabarani akizungumza wakati wa kuuaga mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari wa Kampuni ya Tanzania Daima. 
Mhariri Mtendaji wa kampuni ya Free Media Ltd wanaomiliki gazeti ya Tanzania Daima Absolum Kibanda amesema marehemu Agned Yamo alitumua muda wake kuwaasa kuomba kwa ajili yake.
Kibanda amesema hayo wakati wa kutoa salamu za mwisho kwa marehemu Agnes ambaye alifariki juzi asubuhi kwenye hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam.
Awali salamu mbalimbali zilitolewa zikiwemo kutoka kwa Jukwaa la Wahariri ambapo Katibu wa Jukwaa hilo Bw. Nevile Meena amesema Jukwaa limepoteza mwandishi kijana.
Meena amesema anatufundusha kuwa na mahusiano mema na watu wengi, na pia ametumia fursa hiyo kuwapa pole familia yake na kuongeza kuwa wanaamini Mungu aliyemleta kwa miaka 34  iliyopita ataleta mwingine.
Hata hivyo Kampuni hiyo imegharamia shughuli zote za msiba huku Mtandao wa Waandishi wa Habari ulitoa kiasi cha fedha kama rambirambi.
Aidha Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama kilitoa ubani kwa ajili ya msiba huo.

No comments:

Post a Comment