………………………………………….
Jeshi la polisi mkoa wa Arusha,linawashikilia wanandugu wawili kwa kosa kumpiga na kumsababishia kifo mtu mmoja aliyekuwa na mahusiano ya kimapenzi mtoto wa mmoja ya watuhumiwa hao.
Jeshi la polisi mkoa wa Arusha,linawashikilia wanandugu wawili kwa kosa kumpiga na kumsababishia kifo mtu mmoja aliyekuwa na mahusiano ya kimapenzi mtoto wa mmoja ya watuhumiwa hao.
Kwa mujibu wa kaimu kamanda wa
polisi mkoani,Arusha Akili Mpwapwa,amewataja watuhumiwa kuwa ni Thomas
Leseni(71) na Noel Thomas (60)wakazi wa Njani wilaya ya Arumeru.
Aidha alimtaja marehemu kwa jina
la Pele Charles (30) mkazi wa Njani .Akizungumzia chanzo cha tukio hilo
alisema kuwa marehemu alikuwa na mahusiano na Mary Thomas ambaye ni
mtoto wa Thomas Leseni na mara nyingi amekuwa akimpiga .
Mpwapwa alidai kuwa Marehemu
alikuwa na tabia ya kumpiga binti huyo mara kwa mara na ndipo siku hiyo
watuhumiwa walipopata taarifa na kumfuata marehemu huyo na kuanza
kumpiga kwa fimbo maeneo mbalimbali ya mwili wake na kusababisha kifo
chake.
Marehemu alifariki dunia baada ya
kufikishwa katika hospitali ya west Meru iliyopo Tengeru wilayani
Arumeru baada ya kuvuja damu nyingi
No comments:
Post a Comment