Pages

Tuesday, October 30, 2012

KIONGOZI WA UPINZANI RWANDA AHUKUMI JELA MIAKA NANE JELA.



  
Victoire Ingabire.
 
KIONGOZI wa upinzani nchini Rwanda Victoire Ingabire amehukumiwa miaka minane gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kosa la uhaini.

Viongozi wa mashtaka walitaka afungwe maisha jela kwa kutishia usalama wa nchi.

Mahakama imempata na hatia ya kupuuza mauaji ya Kimbari yaliyotokea mwaka 1994.

Ingabire hakuwa mahakamani wakati hukumu ilipotolewa dhidi yake kwani amekuwa akisusia kuhudhuria vikao vya kusikilizwa kwa kesi hiyo akisema imeshinikizwa kisiasa.

Alikamatwa mwezi Aprili mwaka 2010 na kuzuiwa kushiriki uchaguzi uliofanyika mwaka huo

No comments:

Post a Comment