Pages

Monday, October 8, 2012

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI AMSHANGAA MKANDARASI NA MHANDISI WA SERIKALI KUTOELEWANA MBEYA



NAIBU Waziri wa Uchukuzi Bw.Charles  Tizeba amesema kuwa  kusuasua kwa  mradi uwanjwa wa ndege wa kitaifa wa Songwe jijini Mbeya  kunatokana  na kutokuwepo kwa uelewano baina ya mkandarasi na mhandisi  mshauri na hivyo  kama serikali  wameweka sawa  na  kufanya mabadiliko ya mkandalasi .

Amesema kuwa wamefikia  hatua nzuri ya maelewano na uwanja huo utaanza kukamilika Desemba mwaka huu mapema sana kwa juhudi ambazo sasa serikali imeanza kufanya.

Mwandishi  wa mtandao  huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kutoka Mbeya Esther Macha anaripoti kuwa Naibu waziri huyo ameyasema hayo  wakati alipokuwa akikagua mradi wa uwanja huo na kueleza kuwa utaanza kutumika  pindi yatakapokamilika majengo ya hali ya hewa,usalama wa unga na jengo la abiria na waongoza ndege  ambayo yapo katika hatua za mwisho na serikali haitosubiri mpaka takabaka hilo likamilike na hasara za marudio ya tabala zitakuwa za mkandarasi na si serikali .


Alisema kuwa  juhudi ambazo wamefanya serikali ni kuhakikisha kuwa weanaweka mambo sawa ili kwa wakandarasi hawa kutokuwa na mahusiano mazuri baina yao ,tunachotaka hapa ni uwanja kwenda vizuri na hatua zote zimefanya fanyika.

“Tunategemea kuwa uwanja huu  utawanufaisha watazania zaidi ya milion 1 na utaanza kutumika hata kama mkandarasi ajaweka tabaka la pili na kwamba serikali haitoweza kuvumilia wananchi wake kushindwa kuutumia uwanja huo huku wakiwa na shauku kubwa na kwamba hasara za ukarabati wa tabaka lingine  ni za mkandarasi na si serikali"Alisema.


Hata hivyo alisema mkandarasi anapaswa kufanya jitihada za haraka kuhakikisha  anajitahi kukamilisha  na kwamba endapo kama atafanya uzembe atajikuta akiingia hasara mara mbili kwani ukarabati wa uwanja wakati ndege zinatua unakuwa na gharama kubwa.


Alisema kuwa kutokana na hilo ndege zitaendelea kutua ili kuruhusu shughuli mbalimbali za kijamii kuendelea  na  kuongeza tija ya ukuaji wa uchumi hususan kwa wanambeya ambao wanahitaji kujua hatma ya kukamilika kwa mradi huo.


"Tabaka lililowekwa kwenye sehemu ya ndege kutua limechakachuliwa kwa kiasi kikubwa ni lazima serikali iliangalie hilo  kwani huo ni sehemu ya miradi ya wananchi "Alisema.


Aidha kwa upande mwingine aliwataka wakurugenzi wa viwanja vya ndege kuangalia uwezekano wa kujenga mabwawa ya maji kulingana na mahitaji ya abiria na kwamba wasijenge kwa kufanya makadilio .


"Mnapaswa  kuangalia idadi ya watu wataotumia uwanja huo na viwiane   na mabwawa ya maji na hivyo katika hilo mtakuwa mmefanikisha malengo mliyokusudia"Alisema .

Kwa upande wake   kaimu Mkurugenzi wa viwanja vya ndege Nchi Bw.Suleima Suleiman alisema kuwa hizi ni changamopto zinazojitokeza na kwamba katika hilo watahakikisha mkandarasi anamalizia kazi yake kulingana na mkataba ili uwanja uanze kutumika desemba mwaka huu.


"Nina hakika kazi itakamilika na wananchi kuanza kutumia uwanja wao na kwamba ni jitihada tu zinahitajika na msukumu wa mkandarasi ili kuweza kukamilisha mradi huo.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment