Pages

Tuesday, October 30, 2012

Nape Nnauye:“Tunajivunia ushindi katika Kata 22,tumepoteza Kata Nne Naweza kusema ni sawa na asilimia 75. TLP, ilipata kata moja na CUF kilipata kata moja na Chadema ilipata kata tano





 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akizungmza na waaandishi wa Habari
--
LICHA ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kunyakua viti 22 kati ya 29 vya
udiwani katika uchaguzi uliofanyika juzi, chama hicho tawala kimepoteza
kata nne kilichokuwa kinazishikilia kabla ya uchaguzi huo.

Uchaguzi huo ulifanyika kuziba nafasi zilizoachwa wazi na madiwani walioondoka kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo vifo.

Matokeo
ya uchaguzi huo yanaonyesha kwamba katika Kata 29, Chadema wameshinda
katika kata tano na kukifanya kuongeza madiwani watatu. TLP na CUF kila
kimoja kimepata kata moja.

Kabla ya uchaguzi huo, Chadema kilikuwa na
Kata mbili za Rombo na Mvomero ambazo kimefanikiwa kuzitetea na
kuongeza nyingine tatu, ambazo ni Mlangila (Ludewa), Ipole (Tabora) na
Daraja Mbili (Arusha) ambazo awali, zilikuwa zikishikiliwa na CCM.

TLP
kilitetea kiti chake katika Kata ya Vunjo (Kilimanjaro) wakati CUF
kilitwaa Kata ya Newala ambayo awali ilikuwa ikishikiliwa na CCM.

CCM
kimetetea viti vyake vingine vilivyobaki ambavyo ni Msalato (Dodoma),
Bang’ata (Arumeru Magharibi), Mletele (Songea), Mwawaza (Mjini
Shinyanga), Lwezera (Geita), Bugarama (Kahama) na Bagamoyo mkoani
Pwani.

Viti vingine ni Mnero na Miembeni (Nachingwea), Myovizi
(Mbozi), Mpapa (Momba), Mahenge (Ulanga), Vugiri (Korogwe), Tamota
(Lushoto), Makata (Liwale), Mpepai (Mbinga), Kiloleli (Sikonge), Miyenze
(Tabora), Karitu (Nzega), Lubili (Misungwi), Kilema Kusini (Moshi),
Nanjara/Neha (Rombo), Lokokona (Nanyumbu) na Kitangiri (Newala).

Katika
Kata ya Rwezera, Misango Jeremiah alishinda baada ya kupata kura 1,309
dhidi ya wapinzani wake, Ibuga Mussa (Chadema) aliyepata kura 933 na
Mussa Mtagala (CUC) aliyepata kura 317.  Uchaguzi huo ulifanyika kujaza
nafasi hiyo iliyokuwa wazi baada ya aliyekuwa Diwani wa Kata hiyo,
Anatory Mkufu kufariki dunia kwa ajali ya gari Februari 23, mwaka huu

No comments:

Post a Comment