Pages

Tuesday, October 30, 2012

ORODHA YA NYOTA 23 WANAOWANIA TUZO YA FIFA Ballon d'Or.... AFRIKA NZIMA WAMO DIDIER DROGBA NA YAYA TOURE TU... REAL MADRID YATOA NYOTA SITA, BARCELONA YATOA WACHEZAJI WATANO, MANCHESTER CITY WATATU....!




 ZURICH, Usiwsi
STRAIKA wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi yuko mbioni kuandika rekodi ya kuwa mtu wa kwanza kushinda tuzo ya Mwansoka Bora wa Mwaka wa Dunia kwa mara ya nne mfululizo baada ya kujumuishwa katika orodha iliyotolewa leo na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kuwania tuzo hiyo ya  
Straika huyo mwenye miaka 25, aliyeongeza idadi ya mgoli yake tangu aanze kucheza akiwa na klabu na timu ya taifa hadi kufikia 301 Jumamosi, ni miongoni mwa nyota 23 waliochaguliwa kuwania tuzo hiyo, wengine wakiwa ni hasimu wake, straika wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno,  Cristiano Ronaldo, ambaye alishika nafasi ya pili katika tuzo zilizotolewa mwaka jana na Messi kuibuka kidedea.
Andres Iniesta wa Barcelona, aliyetajwa kuwa mchezaji bora wa fainali za Euro 2012 baada ya kuisaidia Hispania kutwaa ubingwa pia amejumuishwa katika orodha hiyo kama ilivyo kwa Radamel Falcao, ambaye amekuwa akionyesha kiwango cha juu cha upachikaji mabao akiwa na timu yake ya taifa ya Colombia na klabu ya  Atletico Madrid, akiisaidia nchi yake kutwaa ubingwa wa Ligi ya Europa msimu uliopita.
Kocha wa Barca, Tito Vilanova amemwagia sifa Messi wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari leo.
"Sidhani kama tutapata nafasi ya kuona tena mchezaji kama yeye. Sio tu kwa sababu ya mabao anayofunga lakini pia kwa uwezo wake wa kusoma mchezo," alisema kabla ya kumsiofia pia Iniesta.
"Yeye (Iniesta) ni mfano kwa wachezaji wanaolelewa Masia (shule ya soka ya vijana wa Barcelona) na kufikia kiwango cha juu. Ni mchezaji mwingine miongoni mwa wenye viwango vya juu na ambao Barca itapata wakati mgumu wa kuwaibua tena."
Makocha 10 pia wametajwa kuwania Tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka wa Dunia, akiwamo Vicente del Bosque, aliyeiongoza Hispania kutwaa ubingwa wa fainali za Euro 2012 zilizofanyika Julai nchini Ukraine na Poland.
Roberto Di Matteo, aliyetwaa nafasi ya kuiongoza Chelsea miezi miwili kabla ya kutwaa taji la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mwezi Mei, pia amejumuishwa katika orodha hiyo ambayo hata hivyo haikumjumuisha Mfaransa Herve Renard aliyeiongoza Zambia kutwaa ubingwa bila kutarajiwa katika fainali za Kombe Kombe la Mataifa ya Afrika mwezi Februari.
Orodha hiyo fupi itachujwa zaidi na kubaki watu watatu kufikia mwishoni mwa Novemba huku mshindi akitarajiwa kutangazwa duniani kote kupitia matangazo ya moja kwa moja ya televisheni ya sherehe za kukabidhi tuzo zitakazofanyika mjini Zurich, Uswisi Januari 7 mwakani.
Wachezaji (kwa kuzingatia mpangilio wa herufi za majina yao):
1. Sergio Aguero (Argentina)
2. Xabi Alonso (Hispania)
3. Mario Balotelli (Italia)
4. Karim Benzema (Ufaransa)
5. Gianluigi Buffon (Italia)
6. Sergio Busquets (Hispania)
7. Iker Casillas (Hispania)
8. Cristiano Ronaldo (Ureno)
9. Didier Drogba (Ivory Coast)
10. Radamel Falcao (Colombia)
11. Zlatan Ibrahimovic (Sweden)
12. Andres Iniesta (Hispania) 
13. Lionel Messi (Argentina)
14. Manuel Neuer (Ujerumani)
15. Neymar (Brazil)
16. Mesut Ozil (Ujerumani)
17. Gerard Pique (Hispania)
18. Andrea Pirlo (Italia)
19. Sergio Ramos (Hispania) 
20. Wayne Rooney (England)
21. Yaya Toure (Ivory Coast)
22. Robin van Persie (Uholanzi)
23. Xavi (Hispania).
Makocha (kwa kuzingatia herufi za kwanza za majina yao pili):
1. Vicente del Bosque (Hispania/taifa Hispania)
2. Roberto Di Matteo (Italia/Chelsea)
3. Alex Ferguson (Scotland/Manchester United)
4. Pep Guardiola (Hispania/kocha wa zamani Barcelona)
5. Jupp Heynckes (Ujerumani/Bayern Munich)
6. Jurgen Klopp (Ujerumani/Borussia Dortmund)
7. Joachim Low (Ujerumani/taifa Ujerumani)
8. Roberto Mancini (Italia/Manchester City)
9. Jose Mourinho (Ureno/Real Madrid)
10. Cesare Prandelli (Italia/taifa Italia)

No comments:

Post a Comment