Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa Kamishna Jenerali wa
Magereza na maafisa wengine.
Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Peter
Ilomo amesema Rais amemteua Bwana John Casmir Minja (pichani) kuwa Kamishna
Jenerali wa Magereza na kuwateua wengine kuwa maofisa kama ifuatavyo:
·
Dkt. Juma Ally Malewa ameteuliwa kuwa Kamishna, Divisheni ya
Sheria na Uendelezaji wa Magereza.
· Bwana Deonice Lwamahe
Chamulesile ameteuliwa kuwa Kamishna, Huduma za Urekebishaji.
· Bwana Gaston Sanga ameteuliwa kuwa
Kamishna, Divisheni ya Utawala na Fedha.
Wengine ni:
·
Bwana Fidelis M. Mboya ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa
Idara ya Huduma kwa Jamii katika Wizara ya Mambo ya Ndani, ambapo kabla ya
uteuzi huu Bw. Mboya alikuwa Kamishna wa Divisheni ya Sheria na Uendeshaji wa
Magereza na;
· Bwana James B.
Celestine, ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa jamii katika
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, amepandishwa cheo na kuwa Naibu Kamishna wa
Magereza ambapo atarejea Magereza na kupangiwa kazi nyingine.
Kulingana na taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Oktoba 1,
2012 mjini Dar es Salaam na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Peter Ilomo, kupitia
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inasema kuwa uteuzi huu umeanza tangu
tarehe 25 Septemba, 2012.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
1 Oktoba, 2012
No comments:
Post a Comment