Pages

Wednesday, October 3, 2012

RUFAA YA LEMA YASHINDWA KUSIKILIZWA TENA



Na Ashura Mohamed-Arusha
RUFAA  ya  aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema imeshindwa kusikilizwa leo baada ya  kuibuka kwa hoja zaidi ya nne ambazo
zimesababisha kesi hiyo kuahirishwa hadi tarehe itakayopangwa  tena na mahakama ya Rufaa.
Rufaa hiyo imeshindwa kuanza kusikilizwa   baada ya kuibuka kwa hoja nne zilizotolewa na  wakili wa upande wa mashtaka ,Alute Mughwai akisaidiwa na Modest Akida wanaowawakilisha  wajibu rufani ambao ni
Agness Mollel, Happy Kivuyo na Musa Mkanga.
Hoja hizo zilianza kutolewa na  wakili  Mughwai kudai
kuwa rufaa iliyokatwa na Lema kupitia kwa mawakili wake, Method Kimomogoro pamoja na Tundu Lissu imekosewa kwa kukiuka kanuni za mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu pia katika rufaa hiyo hakuna mhuri
wa mahakama wala tarehe .
Mughwai amehoji ni kwanini Lema akimbilie kukata rufaa ndani ya siku 29 badala ya siku 60 kwani hajapitia nakala ya hukumu ya awali hivyo endapo
angepitia hukumu hiyo pamoja na mawakili wake angeweza kujua kuna matatizo gani na ayarekebishe badala yake wamekata rufaa bila
kuangalia kasoro zilizojitokeza.
Alisema ni lazima muhuri wa mahakama uwe pamoja na tarehe na kutokana na umuhumu wa mhuri ndio maana hata mtu wa kijijini anaposhtakiwa au kuhitaji msaada sehemu muhimu inabidi aende kwa mtendaji wa kijiji
kupata barua yenye mhuri na kuhoji ni kwanini Lema amekimbilia kukata rufaa bila kuangalia kasoro zilizopo na kutoa rai kwa jopo la majaji hao kutupilia mbali rufani hiyo ya Lema kwasababu haikakidhi matakwa
ya kisheria.
Nao  Wakili wa Lema ,Method Kimomogolo alisema makosa yaliyotokea ni ya kibinadamu na yamefanywa na mahakama na si Lema wala mawakili wao
hivyo aliwasihi majaji hao kutotupilia mbali rufani yao kwani katika kesi kama hiyo ni lazima makosa madogo madogo yatokee na kusisitiza mahakama kutenda haki kwa Lema

No comments:

Post a Comment