Pages

Tuesday, October 30, 2012

SOMA BARUA YA WAZI KWA RAIS WA DOLA YA ZANZIBAR DK.ALI SHEIN KUTOKA KWA KIONGOZI WA MAIMAMU ZANZIBAR,FARID HADI AHMED



Kiongozi wa Maimamu Zanzibar, Farid Hadi Ahmed 
---
BISMILLAHI ‘RRAHMANI ‘RRAHIM


 Kila sifa njema zinamstahikia Allah, Subhanah wa Taala, 
isofichikakwake dhulma wala harudishi dua ya mwenye kudhulumiwa. 
Rehma na amani zimshukie Mtume Muhmmad (s.a.w) kipenzi chake na
 cha umma, mtetezi wa waliodhulimiwa hata kabla ya kupewa Utume.


Mhishimiwa Rais,Kwa mapenzi makubwa, baada ya kuisoma kwa utulivu 
khutuba yako ya siku tukufu ya Iddil Alfitri, nimelazimika kuandika 
barua hii kufuatana na kauli mbiu ya Mtume Muhammad (s.a.w) inayosema:



“…Dini ni nasaha…nasaha kwa Allah (S.w.T) na ni nasaha kwa Mtume
 (s.a.w.) na kwa viongozi wa Waislamu na kwa watu wote…” 


  Mh. Rais;
Ni kweli nchi yeti ya Zanzibar imechafuliwa jina lake kuwa ni nchi
ya amani kama ilivyogeuzwa nchi yetu na ndugu zetu na kufanywa
kuwa ni koloni lao baada ya mkoloni Mwingereza kutupa uhuru mwaka
1963 na kuwa na kiti chetu Umoja wa Mataifa huku walimwengu wote
wakishuhudia; kiti ambacho kwa uwezo wake Allah atakirejesha
karibuni na wewe ukiwa rais wa Zanzibar au uliyemwakilisha kuweza
kuketi juu yake Insha’allah na sisi wananchi wako wa Zanzibar t
ukifurahikia jambo hilo adhimu.
  Mh.Rais;
Ni kweli nchi yetu inatiwa dosari lakini si kweli kuwa wananchi
wa Zanzibar ndio wanaosababisha dosari hiyo na doa hilo la
uvunjifu wa amani; ushahidi wa maneno haya tutaupata tukirejea
na kutizama kwa jicho la uadilifu na insafu katika matukio
tafauti. Kwa hakika tukifanya hivyo tutagundua bila ya taabu kuwa
 Jeshi la Polisi la Tanzania ndio wahusika wakuu na waanzilishi
wa vurugu na uvunjifu wa amani ya nchi yetu ya Zanzibar
kwa mara zote tatu, nikimaanisha machafuko yaliyotokea tarehe
 25-26/5/2012 mjini Zanzibar na yale ya kuhujumu waumini
na kunajisi misiskiti tarehe 17/6/2012, Donge, Mahonda na
Mkokotoni pamoja na hujuma ya tarehe 20/7/2012 msikitin
pia dhidi ya Waislamu walokusanyika msikiti wa Mbuyuni
 kuwasalia ndugu zao waliofariki kwa ajali ya meli ya
Mv. Skaget. Waislamu tulihujumiwa ndani ya msikiti.

 Jeshi la polisi halikusita hapo bali liliwaingilia  wananchi 
wanyonge mpaka ndani ya nyumba zao na kuwatendea matendo
 haramiya ya chuki na uhuni na katika waliotendewa matendo
 hayo maovu walikuwa wanawake na watoto wachanga. Polisi 
hao wakhalifu wa sharia waharibifu wa amani walifika hadi
 ya kutupa mabomu ya madawa makali ndani ya majumba 
ya raia bila ya kujali athari zitakazowasibu watoto 
wachanga na wanawake wenye kunyonyesha. 

Iwapo jeshi la polisi lililopewa jukumu la kulinda sharia,
 kuweka amani na kuwahami wananchi na mali zao
 ndio wenye kuvunja shariakwa kuwahujumu watu bila ya


  sababu, wananchi na haki zao zitalindwa na nani?


  Mh.Rais;
  Matokeo ya ukiukwaji wa sharia na haki za binadamu 
yaliyopelekea kuiharibia nchi yetu ya Zanzibar sifa yake
 ya amani na utulivu yamesababishwa na jeshi la polisi 
la Tanzania lililoacha kutekeleza wajibu wake wa kutunza
 amani ya nchi yetu Zanzibar . La kusikitisha zaidi ni 
kuwepo baadhi ya watendaji wako wa karibu wanaopotosha
 ukweli na kuifanyia khiyana nchi yetu ya Zanzibar kwa 
kufikisha kwako taarifa za uongo zilizopelekea kuitia doa 
na kuiharibu khutuba yako ilojaa maneno matukufu ya 
Allah Subhanah wa Taala pamoja na mafunzo kutoka 
Sunna za Mtume (s.a.w), khutuba ambayo ilitarajiwa 
kukemea dhulma za jeshi la polisi dhidi ya Waiislam 
na nyumba tukufu za Allah (S.w.T) iliyohujumiwa 
pamoja na wanawake na watoto wachanga ndani
 ya majumba kama ulivotetea makanisa na 
kubainisha hatari na ubaya w walioyachoma
 makanisa hayo kwa lengo la kutaka kuanzisha
fitna baina ya Waislam na jirani zao Wakristo
 waliokaribishwa nchini Zanzibar na kuishi pamoja 
nao miaka mingi kwa amani kiasi ambacho 
haijawahi kutokea Muislamu kulitusi kanisa
 licha kulichoma moto, kwani hayo ni kinyume
 na mafunzo
  ya dini yetu tukufu ya Kiislamu.



  Mh.Rais;   Watu wanaokuwa karibu na Rais ni watu muhimu 
sana katika kufanikisha dhana ya uadilifu na utawala bora
 na wa haki usioogopa kukemea maovu hata kama walotenda 
au kuteleza ni Jeshi la Polisi kwani pia wao ni binaadamu siajabu
 kutenda makosa kwa maksudi seuze kuteleza, Allah Sbhanah wa 
Taala anatwambia: “…Enyi mloamini kuweni wasimamizi wa Allah
 wenye kushuhudia ukweli hata kama ni dhidi ya nafsi zenu…”
 Kwa hivyo, kosa kubwa zaidi ni kuuficha ukweli au kumpotosha 
kiongozi wa nchi hadi kufikia kuwashushia sifa 
wasiostahiki, wahuni ambao waliwatendea ya uhuni na dhulma 
kubwa hata wanawake na watoto.

 Ni khatari wadhulumiwa wanapofikishwa kumshtakia Mfalme wa 
Mbingu na Ardhi juu ya dhulma wanazotendewa. Isitoshe, khiyana
 ya watu kamaa hao wa karibu na viongozi kila inapojikariri 
khiyana hiyo inajenga hisiya kwa wenyeji wa nchi hii ambao 
wengi wao ni Waislamu kuwa wanabaguliwa,  na sio wao tu 
bali hata kudharauliwa nyumba zao tukufu za ibada na 
kuthaminiwa makanisa peke yake. Sisi Waislamu hatutaki
 nyumba zozote za ibada zidharauliwe.Nyumba zote za ibada 
lazima ziwekewe hishima zinazostahiki.




Mh.Rais; 
  Kwa heshma zote naomba zichunguzwe sana sifa mbili kwa
 watu wote wa karibu na viongozi, sifa mbazo ni hatari 
kuzikosa tena zinaweza kuiangamiza nchi yetu tukufu ya 
Zanzibar . Sifa hizo si nyengine illa  ni ukweli na uaminifu 
ambazo ni kinyume na uwongo na khiyana.




Yarabbi Muumba Mbingu na Ardhi, usieshindwa na jambo, 
tunakuomba muhifadhi Rais wetu, turejeshee nchi yetu kwa
 salama na amani, DOLA HURU YA ZANZIBAR, wastiri wanawake
 na watoto wachanga majumbani na Wazanzibari wote 
tunaodhulumiwa kwa kudai uhuru wa nchi yetu ya 


Zanzibar uloporwa na jirani zetu, ndugu zetu baada ya kutoka kwa 
wakoloni.
Amir Mkuu, 
Jumuiya ya Maimamu Zanzibar


  Farid Hadi Ahmed

No comments:

Post a Comment