Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, October 11, 2012

UKITAKA KUTAMBUA UTAJIRI WA OBAMA BILIONI 17 NA DONDOO NYINGINEZO BOFYA HAPA.



 

Mpaka kufikia mwaka 2012 rais huyo wa Marekani alikuwa na utajiri wa Dola za Marekani Milioni 11.8. Sawa na zaidi ya Bilioni 17 za Kitanzania
Vyanzo ya Mapato hayo ni kupitia Vitabu na Siasa.
Mshahara ni dola 400,000 kwa mwaka sawa na Milioni 624 za Kitanzania
Obama ni Rais wa 44 wa Marekani, Mtunzi wa Vitabu na Mtu maarufu zaidi duniani.
Alipokea fedha ya Nishani ya Nobel dola Milioni 1.4 na kuzikabidhi kwenye shughuli za kijamii.
Uamuzi wake wa Kihistoria wa kugombea urais ulimsaidia kuuza mamilioni ya nakala ya Kitabu chake cha “Dreams of My Father and The Audacity of Hope wakati wa kampeni.
Aliuza nakala nyingine 100,000 katika wikialiyochaguliwa.
Mwaka 2009 alipokea advance ya kitabu chake kilichohaririwa cha “Dreams for young adults” mkataba uliomfanya kuwa rais wa kwanza aliyeko madarakani kupokea advance ya vitabu.
Mshara kamili wa Obama ni dola 400,000 kwa mwaka, lakini pia pia anaweza kutumia akaunti ya matumizi ya dola 150,000 sambamba akaunti isiyokatwa kodi kwa ajili ya kusafiri ya dola 100,000 na bajeti ya burudani ya dola 20,000.
Obama alikuwa Seneta wa Jimbo la Illinois kwa mihula mitatu na kuwa mtu wa kwanza mwenye Asili ya African American kuwa rais wa Marekani.
Barack Obama alizaliwa August 4, 1961 huko Honolulu, Hawaii, na Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Columbia na Shule ya Sheria ya Harvard

No comments:

Post a Comment