Mbali na Mauaji hayo pia askari polisi mwenye namba G.406 Pc Lameck alijeruhiwa kwa risasi katika mguu wa kushoto huku walinzi watatu wakijeruhiwa kwa mapanga wakati wakijaribu kukoa mali zilizoporwa katika duka hilo .
Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Bw.Robert Boaz amethibitisha kutokea kwa tukio hilo majira ya saa 7 usiku wa kuamkia leo baada ya kuvamia duka la Bw. Gaudence Temu na kuiba vifaa mbalimbali vya ujenzi.
Akielezea mazingira ya tukio hilo kamanda Boaz alisema kundi la majambazi watano walivamia dukani kwa Gaudence Temu na kumjeruhi kwa sime mlinzi aitwaye Hamis Juma (25) na kisha kuiba.
Alisema kufuatia tukio hilo walinzi wa sungusungu Richard Temu na Erick Yuda walijitokeza ili kutoa msaada lakini nao walishambuliwa kwa mapanga na kujeruhiwa na wote wamelazwa katika hospitali ya Kilema.
Kwa mujibu wa kamanda Boaz baada ya tukio hilo taarifa za uvamizi zilifikishwa polisi na
askari wa doria walikwenda haraka eneo la tukio kutoa msaada na kuanza
kuwasaka majambazi hao ambao walitokomea mara baada ya tukio hilo.
Alisema
ufuatiliaji wa kina ulifanyika na kubaini maficho ya majambazi hao
ambayo ni nyumba ya mmoja wao iliyopo kijiji cha Kyara eneo la Marangu,
ambapo askari walikwenda na baada ya kufika waliwataka wafungue mlango na kujisalimisha lakini hawakutaka hadi Bomu la machozi lilipotupwa katika nyumba hiyo.
Alisema mara baada ya Bomu la machozi kutupwa majambazi hao walitoka nje huku wakirusha risasi ambapo chembechembe za risasi zilimjeruhi skari mmoja ambaye ni Pc Lameck kwenye mguu wa kushoto.
“Askari nao walijibu mapigo na kufanikiwa kuwapiga risasi na kuwaua majambazi watano waliojaribu kutoroka kutoka kwenye nyumba hiyo”alisema kamanda.
Aidha
aliwataja majambazi hao kuwa ni Paul Baltazari Bahati (25) ambaye ni
mwenye nyumba, Remius Msambure kwa jina maarufu mreno (30) ,Focus Daud
Mtui ( kwa jina maarufu Kisinja (35) wote wakazi w kijiji cha Kitowo
Marangu,Elia aliyetambulika kwa jina moja mmasai mkazi wa kijiji cha Msitu wa Tembo na mmoja bado hajatambulika.
Kamanda alisema katika eneo la tukio ilikutwa bunduki moja aina ya Shortgun greener yenye No. 858356 na risasi nne, maganda ya risasi ambapo bunduki hiyo iliibwa Tarehe septemba 15 mwaka huu katika kijiji cha Chemchem wilaya ya Moshi kwa Bw. Kribia Bwanakule Mmari.
Vingine ni Pistol aina ya Browning ambayo imefutwa namba na
risasi mbili,Risasi 10 za bunduki aina ya SMG,Mapanga,sime,yenye damu,
Brief case yenye mabomba ya sindano,sindano, uzi wa kushonea majeraha
hospitali,zana mbalimbali za kuvunjia pamoja na mali mbalimbali za wizi.
Hata
hivyo baadhi ya wakazi wa moshi wamepongeza hatua ya jeshi hilo na
kusema kuwa majambazi hao wamekuwa kero katika kijiji hicho kwa muda
mrefu hali ambayo ilikuwa ikiwanyima usingizi kwa kuhofia kuvamiwa.
No comments:
Post a Comment