Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, November 18, 2012

AL AHLY MABINGWA AFRIKA, WAWAKUNG'UTA ESPERANCE KWAO



Football | CAF Champions League

Mohamed Nagui 

Al Ahli take African Champions League



MABAO ya Mohamed Nagui na Walid Soliman usiku huu yameipa Al Ahly ya Misri taji la Ligi ya Mabingwa Afrika kufuatia ushindi wa mabao 2-1 ugenini dhidi ya wenyeji na waliokuwa watetezi wa taji, Esperance ya Tunisia.
Hilo linakuwa taji la saba  na kuifanya klabu hiyo ya Misri iendelee kuwa klabu iliyotwaa mara nyingi zaidi taji hilo.
Ahly imetwaa taji hilo kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2..
El Sayed Hamdi, alimtoka beki Walid Hichri na kuingia kwenye eneo la penalti akitokea wingi ya kushoto na kumsetia bao la ufunguzi Nagui dakika mbili kabla ya mapumziko.
Soliman alitengeneza 2-0 kwa shuti dhaifu ambalo mabeki wa Esperance walishindwa kuzia na tangu hapo mambo yakawa magumu kwao,kwani walitakiwa kushinda mabao matatu, lakini wapata moja la kufutia machozi lililotiwa kimiani na Yannick Ndjeng.

No comments:

Post a Comment