Ni kuhusu elimu bure hadi sekondari, asema iwe moja ya ajenda za ccm 2015
WAZIRI
Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema wakati umefika kwa sasa hapa
nchini elimu ya Sekondari iwe elimu bure na kumwondolea mwananchi wa
kawaida mzigo wa kubeba gharama za elimu hiyo.
Lowassa
akizungumza jana mjini Babati alisema, mjadala kuhusu elimu kutolewa
bure hadi sekondari haukwepeki, hivyo kuwataka wadau wa elimu kuanza
sasa kujadili suala hilo na kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapaswa
kulifanya hilo kuwa moja ya ajenda zake katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Alisema
elimu ya sekondari ikifanywa bure, itakuwa ni fursa kwa kila mtoto wa
Kitanzania kuipata. Hatua ambayo itaongeza weledi na uelewa wa mambo
mengi katika jamii.
“Ninasema
sasa wakati umefika elimu ya sekondari kuwa kama elimu ya msingi kwa
watoto kusoma bure kuanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha nne,”
alisisitiza Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli (CCM).
Kwa kauli
hiyo, Lowassa ni kama ameunga mkono Sera ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) ambao waliingia katika mgogoro na CCM kuhusu elimu
kutolewa bure wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2010.
Chadema
wamekuwa wakisisitiza kwamba elimu bure inawezekana hadi ngazi ya
sekondari, lakini wakati wote CCM wamekuwa wakisema kuwa suala hilo
haliwezekani na kwamba kauli za aina hiyo ni kuwahadaa wananchi.
Katika
Uchaguzi Mkuu wa 2010, aliyekuwa mgombea wa urais kupitia Chadema, Dk
Willibrod Slaa alitumia sera ya elimu bure kuanzia chekechea hadi
sekondari kama kete ya kusaka ushindi, huku akisema chama chake
kingetenga asilimia 35 ya bajeti kwa ajili ya kuboresha elimu na kutoa
elimu bure.
Hata
hivyo, aliyekuwa mgombea wa CCM na baadaye kupata ushindi, Rais Rais
Jakaya Kikwete alikuwa akiwatahadharisha wapigakura kuwa kwamba ahadi ya
Chadema ni hewa na kwamba hilo lisingewezekana.
Mvutano
huo uliwaingiza makada wengine ambao ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman
Kinana ambaye wakati huo alikuwa Meneja Kampeni wa CCM na Waziri wa
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta na kwa upande wa Chadema,
Dk Kitila Mkumbo naye alijitokeza kutetea sera ya chama chake.
Katika
mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika Novemba 10, 2010 katika Kata ya
Mchangimbore katika Jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma, Rais Kikwete
alisema “Serikali haiwezi kutoa huduma za jamii bure” na kwamba lazima
wananchi wachangie.
“Nimebahatika
kukaa serikalini muda mrefu hiyo sera ya bure tulijaribu na ikatushinda
na wakati huo Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, tulikaa naye
tukaona hilo haliwezekani tukaamua tubadilishe sasa nawashangaa wenzetu
wanawadanganya eti watatoa bure.”
Kwa
upande wake Dk Slaa akiwa mjini Arusha katika moja ya mikutano yake
alisema kwamba CCM walikuwa wakipinga sera ya elimu bure hadi sekondari
kutokana na kulea ubadhirifu na kuthamini anasa kuliko maendeleo kwa
wananchi.
Kauli ya Lowassa
Jana akizungumza muda mfupi kabla ya kuanza kuendesha harambee ya ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Babati, Lowassa alisema wakati umefika kwa kila Mtanzania kuzungumzia suala hilo bila ya woga.
Kauli ya Lowassa
Jana akizungumza muda mfupi kabla ya kuanza kuendesha harambee ya ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Babati, Lowassa alisema wakati umefika kwa kila Mtanzania kuzungumzia suala hilo bila ya woga.
No comments:
Post a Comment