Football | Barclays Premier League
| |
United, ilipoteza mechi ya tatu msimu huu Uwanja wa Carrow Road, kwa bao la dakika ya 60 lililofungwa kwa kichwa na mchezaji wao wa zamani wa timu yao ya vijana, Anthony Pilkington.
Chelsea imefungwa 2-1 na West Brom, bao lililowamaliza likifungwa na Peter Odemwingie kipindi cha pili.
Ushindi wa City Uwanja wa Etihad ulitokana na mabao ya Muargentina Sergio Aguero na Carlos Tevez, na kupanda kileleni mwa Ligi Kuu kwa mara ya kwanza msimu huu.
Vijana wa Roberto Mancini sasa wana pointi 28, baada ya kucheza mechi 12, huku wapinzani wao, United wakiwa nafasi ya pili kwa pointi zao 27.
Chelsea ina pointi 24 kutokana na mechi zao 12.
No comments:
Post a Comment