MKURUGENZI Mkuu
wa Shirika la Habari, BBC, George Entwistle amejiuzulu wadhifa huo.
George Entwistle amejiuzulu kama Mkurugenzi BBC kwa kile kufanyika
makosa katika moja ya vipindi vya shirika hilo la habari Ulimwenguni.
Taarifa zaidi zinasema Entwistle amekuwa akishutumiwa kwa namna
alivyoshughulikia taarifa iliyopeperushwa katika kipindi cha Newsnight.
Taarifa
hiyo kwa makosa ilimshutumu aliyekuwa Waziri wa Fedha wakati wa serikali
ya Conservative, Lord McAlpine, kwamba alihusika katika kashfa ya
kudhalilisha watoto. Tayari shirika la BBC limekuwa likichunguzwa vikali
katika kashfa inayomhusu mtangazaji wake wa zamani Jimmy Savile kwa
madai ya kuwadhalilisha watoto.
Kipindi
hicho cha Newsnight kinadaiwa kuacha kwa makusudi kutangaza habari ya
uchunguzi kuhusiana na kashfa ya Bwana Savile. Wakati wa kutangaza
kujiuzulu Jumamosi, usiku Entwistle alisema; “ilikuwa ndilo jambo la
heshima kwangu kulifanya”.
Akisimama
kando yake Mwenyekiti wa BBC Trust, Lord Patten alisema; “huu ulikuwa
moja wapo ya usiku wa majozi katika maisha yangu ya umma”. “Muhimu kwa
BBC ni jukumu lake kama chombo cha habari kinachoaminika”
“Kama
Mhariri Mkuu wa shirika hili la habari, kwa heshima kubwa George
amediriki kujiuzulu kutokana na makosa yasiokubalika – uanahabari mbovu
ambayo umezua malalamiko mengi”.
No comments:
Post a Comment