Pages

Friday, November 23, 2012

Mwakyembe atoa amri: Wafanyakazi wote walio kwenye wizara yake wasitumie daraja la kwanza kwenye ndege



Mh. Dr Mwakyembe
IKIWA NI SIKU CHACHE tokea aunde bodi mpya ya watu wanane Mamlaka ya Bandari [TPA] watakaoanza kazi rasmi Januari mwakani, ametoa agizo lingine kali kwa wafanyakazi wa Wizara hiyo

Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe amewaagiza wafanyakazi wote waliochini yake kutosafiri kwa kutumia daraja la kwanza kupitia usafiri a ndege popote waendapo ili kudhibiti matumizi mabovu ya fedha za umma

Agizo hilo lilitolewa jana akiwa mkoani Tanga mbele ya vyombo vya habari na kusema wafanyakazi wote wa serikali walioko chini ya wizara yake ni marufuku kusafiri kwa ndege kwa kutumia daraja la kwanza

Amesema mfanyakazi yeyote atakayekaidi agizo hilo fedha zake zitakatwa kwenye malipo yake ya mwezi ikiwa ni kupunguza ama kuondoa matumizi mabovu ya fedha za serikali na kufafanua anayetakiwa kutumia daraja hilo ni Rais pekee

Vilevile aliweza kuviambia vyombo vya habari kuwa, anakusudia kuleta mageuzi katika sekta ya usafirishaji katika bandari (PTA) ili kuweza kuleta ushindani wa kibiashara na nchi jirani ili waweze kutumia bandri za hapa nchini kinyume na ilivyo sasa

No comments:

Post a Comment