Pages

Friday, November 23, 2012

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AWASILI MKOANI KATAVI TAYARI KWA UZINDUZI RASMI WA MKOA HUO



Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutegwe mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda leo mchana kwa ajili ya kushiriki katika shughuli ya uzinduzi rasmi wa mkoa huo utakaofanyika siku ya jumapili kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda, mkoa huo ukizunduliwa rasmi kwa ving'ola na Mh Dkt. Gharib Bilal Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania anayetarajiwa kuwasili kesho mjini Mpanda tayari kwa ajili ya uzinduzi huo
Waziri Mkuu Mizengo Pinda viongozi mbalimbali wa CCM baada ya kuwasili mkoani Katavi leo mchana katikati ni Waziri wa Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu na kulia ni Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rtengwe.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na Mbunge wa Mpanda Mjini, Said Arfi (Chadema) mara baada ya kuwasili mjini Mpanda leo
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe kwa ajili ya kukagua vikundi vya ngoma katika uwanja wa ndege wa Mpanda mara baada ya kuwasili, kushoto ni mke wake mama Tunu Pinda.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda kushoto akifurahia jambo na Dkt. Mary Nagu waziri wa Uwezehaji Ofisi ya Waziri Mkuu wakati walipowasili katika uwanja wa ndege wa mpanda leo mchana.
Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda akuwapungia mkono wakazi wa mjini Mpanda waliofika uwanja wa ndege kumlaki , kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe.
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza wakati wa mapokezi ya Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda katika uwanja wa ndege wa Mpanda.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa Mpanda Mjini, Said Arfi (Chadema) wakati wa mapokezi ya waziri kuu Mizengo Pinda mjini Mpanda, Mh. Rajab Rutengwe anatoa kauli mbiu yake kuwa "SIASA NI MAENDELEO".

Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajabu Rutengwe akimsiliza Kamanda wa polisi Mkoa wa Katavi kamanda Dhahiri Kidavashari wakati akimpa maelezo ya utaratibu wa mapokezi ya mgeni huyo, kulia anayesikiliza kwa makini ni Afisa Habari wa mkoa wa Rukwa Bw. Hamza Temba
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea banda la Mkoa wa Rukwa ili kupata maelezo kadhaa katika maonyesho hayo kulia ni Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt Rajab Rutengwe na kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipata maelezo katika banda la mkoa wa Rukwa katikati ni Mke wake Mama Tunu Pinda.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa maafisa wa ardhi katika mkoa wa Katavi mara baada ya kutembelea banda la mkoa huo.
Benki ya NMB nao wanashiriki katika uzinduzi wa mkoa huo kama wanavyoonekana wafanyakazi wa benki hiyo wakiwa katika banda lao kutoka kulia ni Hussein Kabwe, Berdon Mwakatobe na Aneth Nyakiboha.
Afisa habari wa Shirika la nyumba NHC akitoa maelezo kwa Mhadhiri katika chuo kikuu cha Dar es salaam John Kafuku wakati alipotembelea katika Banda la shirika hilo
Banda la Kampuni ya Simu ya TTCL wafanyakazi wakiwa katika pilika mbalimbali za kuandaa shughuli zao katika banda hilo kutoka kulia ni Alinamaka Ndalima, Humphrey Ngowi na Thomas Lemunge.
Bendi kutoka mkoani Katavi ikitoa burudani katika maonyesho hayo huku ikipigwa tafu na mwanamuziki kongwe Bw. Hamza Kalala ambaye yuko huko kwa ajili ya kuinoa bendi hiyo.
Mwanamuziki Hamza Kalala akifanya vitu vyake katika maonyesho hayo ambayo yanaambatana na uzinduzi wa mkoa wa Katavi siku ya jumapili Novemba 25 mjini Mpanda.PICHA NA FULLSHANGWEBLOG.COM

No comments:

Post a Comment