YANGA
imethibitisha kwamba straika wake, Said Bahanuzi pamoja na beki Nadir
Cannavaro wataondoka leo Jumanne jioni kwenda Shanghai, China kwa
majaribio lakini Haruna Niyonzima 'Fabregas' akili yake ipo Ubelgiji.
Ingawa wachezaji hao walifanya siri, Mwenyekiti wa Kamati ya
Mashindano, Abdallah Bin Kleb alithibitisha kwamba wanakwenda kwenye
klabu moja ya daraja la pili na watakaa huko wiki mbili na wamewaruhusu
kwa kuwa ligi imesimama.
"Kama wakifuzu tutakaa chini tujadiliane na tujue wanahitajika lini
na sisi tutanufaika vipi na wachezaji wenyewe watanufaika vipi
kimaisha," alisema Bin Kleb akidai kwamba bado wanahitajika Jangwani
lakini Wachina wakipanda dau watawaachia kwa maslahi yao na nchi.
Haruna kwa upande wake alisema: "Naweza kuondoka wakati wowote
kuanzia sasa kwenda Ubelgiji na sasa nasikilizia mpango huo na nafikiri
uko katika hatua za mwisho, mipango itakapokamilika nitasubiri ruhusa ya
viongozi kwani wao ndiyo wenye uamuzi wa mwisho kwa sababu mimi bado ni
mchezaji wa Yanga."
Akikizungumzia kikosi cha Yanga, Fabregas alisema: "Tusibweteke
tujiandae kila mmoja kwa nafasi yake ili tufanye vizuri mzunguko wa pili
wa Ligi Kuu Bara."
No comments:
Post a Comment