Rais Yoweri Museveni wa Uganda amekuwa Mwenyekiti Mpya wa Ukanda wa Kiuchumi wa Nchi za Afrika Mashariki na Kusini (COMESA).
Rais Museveni amechukua wadhfa huo kutoka kwa rais wa Malawi Joyce Banda aliyemaliza muda wake, ambaye amekabidhi nafasi hiyo katika Mkutano wa 16 unaoshirikisha wakuu wa nchi na serikali wa COMESA.
Katika Mkutano huo unaofanyika nchini Uganda na unaotarajiwa kumalizika leo, Rais Museveni katika hotuba yake amesema uchumi wa nchi za kiafrika umegawanyika mno, kitu ambacho kinadhoofisha ukuaji wake na kupelekea nchi hizo kushindwa kuvutia wawekezaji wa kigeni.
Amesema upo umuhimu wa kuwa na umoja wa kibiashara kwa nchi za Afrika.