Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, November 25, 2012

REFA ALIYEIBEBA MANCHESTR CITY ILIPOCHEZA NA REAL MADRID ATOSWA KATIKA HATUA YA 16-BORA UEFA...!




Gianluca Rocchi
Gianluca Rocchi akimlima kadi nyekundu beki Alvaro Albeloa wa
 Real Madrid kabla ya kuamuru kupigwa kwa penati iliyofungwa
 na Sergio Aguerro wa Man City wakati wa mechi yao ya Kundi
D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya juzi Jumatano, Novemba 21, 2012.
Kushoto ni Xabi Alonso
MADRID, Hispania
Uchezeshaji uliojaa utata wa refa Gianluca Rocchi wakati wa mechi ya 

Kundi D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kati ya Manchester City na 

Real Madrid haujaachwa bure na Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA) 

baada ya mwamuzi huyo kutoswa katika orodha ya marefa 

watakaochezesha mechi za mtoano hatua ya 16-Bora ya michuano hiyo.

Huku Pierluigi Collina akiwa ndiye bosi wa Kamati ya Waamuzi ya 

UEFA kwa sasa, kamwe Rocchi hakutarajiwa kupona katika panga 

kali la refa huyo mstaafu aliyejitwalia umaarufu mkubwa enzi zake.

 Na sasa, Rocchi amepigwa chini pamoja na marefa wengine wawili 

walioonekana kuchemsha kama yeye ambao ni Tagliavento na Rizzolli.

Licha ya kuondoshwa katika orodha ya marefa watakaochezesha 

hatua ya 16-Bora ya UEFA, Rocchi pia atashushwa daraja na msimu 

ujao anawexza kupangwa katika Ligi ya Europa na kamwe siyo tena 

katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Katika tukio mojawapo la kukumbukwa, Rocchi alipeta faulo 

ya wazi aliyofanyiwa Ronaldo wakati akiwatoka kwa kasi 

mabeki wa Man City, tukio lililowashangaza wengi na 

kuwakasirisha Ronaldo na kocha wake Jose Mourinho 

walioonekana wakilalamika mfululizo kwa kurusha mikono hewani.

Mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya 1-1, bao la Real Madrid 

likifungwa na Karim Benzema aliyeunganisha vyema krosi kali 

ya Angel Di Maria na wenyeji Man Cioty wakasawazisha kupitia 

penati iliyowekwa wavuni na Sergio Aguero; adhabi ambayo pia

 iliambantana na kadi nyekundu kwa beki Alvaro Albeloa wa 

Real Madrid. Sare hiyo iliivusha Madrid kwa hatrua ya 16-

Bora huku Man City ikitolewa rasmi.

No comments:

Post a Comment