skip to main |
skip to sidebar
TETESI ZA KUWEPO MISUKULE IRINGA ZASIMAMISHA SHUGHULI ,POLISI WAFIKA KUTAWANYA WANANCHI -
polisi wakiwasaka vijana walioeneza uvumi wa kuwepo kwa msukule eneo la Mwangata mjini Iringa sasa
wananchi wakiwa wamesitisha shughuli zao kutaka kuona msukule unaodaiwa kuonekana
Polisi wakiwa katika msako wa kuwasaka wazushi wa taarifa hiyo ya kuonekana mtoto anayedaiwa kufa siku nyingi a.k.a Msukule
Polisi wakiwa katika msako eneo la Mwangata
Zimezuka
habari zenye utata ambazo mtandao huu bado kuthibitisha kuwa kuna
mtoto anayedaiwa kufa na kuzikwa kuonekana leo akidaiwa kuwekwa Msukule
.
Tukio hilo limetokea eneo la Mwangata mjini Iringa na
kupelekea polisi kufika kuwatawanya wananchi hao na kuwasaka wale
ambao wanadaiwa kueneza uvumi huo.
Hata hivyo hakuna mwananchi
hata mmoja kati ya waliokuwepo hapo ambaye amethibitisha kuona
msukule huyo zaidi ya kila mmoja kusema amesikia .
Wananchi hao wameizunguka moja kati ya nyumba eneo hilo wakitaka kuichoma moto kwa madai kuwa ndani kuna msukule huyo.
Rai
ya mtandao huu kwa jamii ya mkoa wa Iringa na Tanzania kwa ujumla
kuepuka kuamini imani za kishirikina ambazo zinaweza kuvuruga amani
yetu
No comments:
Post a Comment