Pages

Friday, November 23, 2012

WAHADHIRI CHUO KIKUU KAMPALA (KIU) DAR WAGOMA KUDAI MISHAHARA YAO






Kampala International University
HABARI kutoka Chuo Kikuu cha Kampala Tawi la Dar es Salaam Tanzania, zinapasha kuwa Wahadhiri na wafanyakazi wa Kawaida wa chuo hicho wameingia katika mgomo kuanzia leo.



Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa baadhi ya wanafunzi chuoni hapo na kuifikia meza ya Father Kidevu Blog, wanadai kuwa Wahadhiri hao wameanza mgomo wao leo wa kutoingia madarasani kufundisha kufuatia madai yao ya mishahara na posho nyingine.



Wanafunzi hao ambao hawakupenda kutajwa majina yao wanasema kuwa walihao walikaa kikao jana na kufikia muaafaka huo wa kuingia katika mgomo wa kudai mishara yao na hawatoingia madarasani hadi pale watakapolipwa fedha zao hizo.



“Awali tulikuwa tukisikia kuwa wanadai mishara ya miezi mitano yaani tangu mwezi mei hawajalipwa lakini kwa mujibu wa taarifa zilizo samba chuoni hapo leo ni kuwa madai ya wahadhiri hao yalioyobaki hadi sasa ni ya miezi miwili.” Alisema Mwanafunzi huyo.  



Wanafunzi hao walidai kuwa kuwepo kwa mgomo huo kutawaathiri kimasomo kwani wapo baadhi yao wanaoingia katika kufanya mitihani hivi karibuni na wanafunzi wa mwaka wa kwanza ndio kwanza wameripoti chuoni hapo hivyo wanahitaji kupata mafunzo zaidi na si kukutana na migomo hiyo.

No comments:

Post a Comment